CHEKA TARATIBU...

Mchungaji mmoja katika siku za mwanzoni za utumishi wake kafika kwenye mji mmoja mdogo maeneo ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kuhubiri Neno la Mungu. Siku moja akiwa anataka kutuma barua, akamuuliza mtoto mmoja barabara inayoelekea ziliko Ofisi za Posta. Baada ya mtoto yule kumwelekeza, Mchungaji akamshukuru sana na kusema, "Kama utakuja kanisani leo jioni, utanisikia nikimweleza kila mtu jinsi ya kwenda peponi."
Yule mtoto akajibu, "Sitakuja kabisaaa! Wewe mwenyewe hujui hata njia ya kwenda Ofisi za Posta!" Balaa...

No comments: