CHEKA TARATIBU...

Jamaa watatu wako kwenye usaili kwa ajili ya kupelekwa sayari ya Mars. Nafasi ilikuwa moja tu ambapo atakayekwenda hatorudi tena duniani.
Mtahiniwa wa kwanza Injinia, akaulizwa anataka kulipwa Shilingi ngapi kwa safari hiyo. Akajibu, "Shilingi milioni moja, maana yote nataka kununulia kamera ya kwenda nayo huko."
Mtahiniwa aliyefuatia ni Daktari, naye akaulizwa swali hilo hilo. Akajibu, "Shilingi milioni mbili, sababu nataka kuiachia familia yangu."
Mtahiniwa wa mwisho alikuwa Mwanasheria. Yeye alipoulizwa anataka kulipwa kiasi gani akaenda moja kwa moja kwa muuliza swali na kumnong'oneza sikioni, "Shilingi milioni tatu."
Akaulizwa, "Kwanini nyingi hivyo kuliko wenzako waliotangulia?" Mwanasheria akajibu, "Kama ukinipa milioni tatu, nitakukatia wewe milioni moja, mie pia nitabaki na milioni moja, halafu tutampa Injinia iliyobaki aende hiyo safari!"

No comments: