CHEKA TARATIBU...

Gari moja imesababisha ajali mtaani na kutokomea. Kama ilivyozoeleka umati mkubwa sana wa watu ukazingira eneo la ajali. Mwandishi wa habari akawa anataka kuandika kilichotokea lakini akashindwa kabisa sehemu ya kupita. Haraka akapata akili na kupiga makelele, "Jamani nipisheni, nipisheni mimi ni mtoto wake!" Watu wakampisha na alipofika karibu kumbe alikuwa kagongwa Mbwa! Duh…

No comments: