CHEKA TARATIBU...

Jamaa watatu wamekufa na moja kwa moja wakafika kwenye geti la kuingilia peponi. Pale wakakuta sharti la kuingia humo ni lazima kila mmoja atoe zawadi inayohusiana na Krismasi.
Wa kwanza akajipapasa mifukoni na kutoa mti wa Krismasi, hivyo akaruhusiwa kuingia.
Wa pili akatoa mkate mkavu, naye pia akaruhusiwa kuingia.
Wa mwisho akakabidhi soksi ndefu.
Huku akiwa amechanganyikiwa, Mtakatifu Petro akauliza, "Hii inahusika vipi na Krismasi?"
Jamaa akajibu, "Hizi ni za mwimbaji wa wimbo wa Krismasi." Duh, balaa...

No comments: