CHEKA TARATIBU...

Mama mmoja kapanda basi akiwa amembeba mtoto wake ndipo kondakta akasema: "Duh, huyo ni mtoto mwenye sura mbaya kuliko wote niliowahi kuwaona."
Akiwa kakasirika, mama yule akatupia hela yake ya nauli kwa dereva kisha akapita kati ya viti na kukaa mbele kwenye basi. Jamaa aliyekaa karibu alijua jinsi mama yule alivyofadhaika ndipo akamuuliza kulikoni?
Mama akajibu kwa hasira, "Kondakta kanitukana." Yule jamaa kwa masikitiko akaanza kumfariji, "Kafanya makosa sana, kondakta hatakiwi kabisa kumtukana abiria wake anayemlipa nauli." Mama akadakia, "Ni kweli kabisa! Nadhani wacha nimfuate nikamzabe japo vibao viwili ashike adabu!" Jamaa akajibu kwa upole huku akimpokea mtoto yule mama, "Hebu nipe huyo nyani nikushikie!" Duh, kasheshe…

No comments: