CHEKA TARATIBU...

Mfungwa kapokea barua kutoka kwa mkewe. Mke kauliza kwenye barua hiyo, "Nimeamua kupanda mihogo kwenye bustani nyuma ya nyumba. Wakati gani mzuri kufanya hivyo?"
Huku akijua kwamba askari jela huwa wanazisoma barua zote, yule mfungwa akajibu, "Mke wangu mpenzi, fanya chochote lakini usifukue bustani ya nyuma ya nyumba! Kule ndiko nilikofukia zile kilo 20 za dawa za kulevya."
Wiki moja baadaye akapokea barua nyingine kutoka kwa mkewe ikisema, "Huwezi kuamini kuna watu wamekuja na majembe na kulima bustani yote nyuma ya nyumba."
Mfungwa akaandika kwenye barua nyingine, "Mke wangu mpenzi, sasa ndio wakati mzuri wa kupanda hiyo mihogo!"

No comments: