CHEKA TARATIBU...

Binti mmoja mwanafunzi wa chuo baada ya kuelemewa na masomo kaamua kutafuta njia ya mkato ya kufaulu mitihani yake. Asubuhi na mapema akamvamia Profesa wake kijana chumbani na kueleza shida yake.
Akaanza huku akipiga magoti mbele ya Profesa, "Profesa niko tayari kufanya chochote ili tu nifaulu mitihani yangu."
Profesa akajibu, "Chochote?" Binti akajibu kwa msisitizo, "Chochote kile Profesa nitafanya!" Baada ya kufikiri kwa muda Profesa akamwambia, "Nenda kasome kwa bidii!" Duh...

No comments: