CHEKA TARATIBU...

Tajiri mmoja wa kupindukia kaenda nyumbani kwa Mchungaji na kuomba kuonana na mke wa mchungaji ambaye ni maarufu sana kwa kutoa misaada kwa wasiojiweza.
Alipofika jamaa akaanza kusema, "Mama nimekuja kukupa taarifa za kuhuzunisha kuhusu familia moja hapa mtaani. Baba yao kafariki, mama anaumwa ile mbaya, na watoto tisa wanataabika. Mabaya zaidi ni kuwa wanakaribia kulala nje mtaani kukosa Shilingi 40,000 za kodi ya nyumba."
Mama Mchungaji akajibu, "Doh, inasikitisha sana! Nataka kujua wewe ni nani hasa?"
Huku akitoa kitambaa na kujifuta jasho Tajiri akajibu, "Mimi ndio mmiliki wa nyumba hiyo!"

No comments: