CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja kampenda sana mwanamke, lakini alikuwa na aibu sana kumweleza dada huyo kwamba anataka kumuoa. Wakafikisha miaka sita kila mmoja akiwa hajaoa wala kuolewa. Katika kipindi chote hicho walikuwa wakihusiana kila wiki mara moja lakini alishindwa kueleza nia yake ya kumuoa. Siku moja jamaa akaamua kuvunja ukimya na kumpigia simu, "Mary!" Mwanamke akaitikia, "Ndio, Mary ninaongea!" Jamaa akaendelea, "Uko tayari kuolewa nami?" Mwanamke akajibu, "Hakuna shida, niko tayari. Samahani, nani unayeongea sasa?" Kaazi kweli...

No comments: