Wawekezaji
wa Marekani wameonesha nia ya kutaka kuwekeza kwenye maeneo ya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji
nchini (EPZA).
Mkurugenzi
Mkuu wa EPZA, Dk Adelhelm Meru alisema hatua hiyo, inadhihirisha matunda ya
kongamano la masuala ya biashara, lililofanyika Marekani mwezi huu yanaanza kuonekana.
Kongamano
hilo lilifanyika baada ya Rais Jakaya Kikwete kushiriki mkutano wa Marais wa
Afrika na Rais Barack Obama wa Marekani jijini Washington D.C.
Kongamano
hilo lililojulikana kama ‘Doing Business in Tanzania’ liliandaliwa na EPZA,
Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na Kituo cha Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa
kushirikiana na Corporate Council on Africa ya Marekani.
“Katika
siku chache baada ya kurejea, tumepata kampuni tatu ambazo zimeleta maombi ya
nia ya moja kwa moja kuwekeza katika maeneo maalumu,” alisema.
Alisema
mamlaka imepokea maombi yanayotaka kuwekeza katika maeneo ya kuongezwa thamani
zao la ngozi, teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) na ujenzi wa
miundombinu katika maeeneo maalumu ya mamlaka.
Akifafanua,
alisema matarajio yaliyopo kwa sasa ni kuendelea kupata wawekezaji wengi kutoka
nchi hiyo, kwa vile kongamano hilo liliipa nafasi nzuri Tanzania kutangaza
fursa zilizopo nchini.
Rais Jakaya
Kikwete aliongoza ujumbe wa Tanzania katika kongamano hilo kubwa. “Walionesha
nia ya kutaka kuwekeza katika maeneo ya viwanda vya kuongeza thamani mazao ya
Kilimo na uzalishaji nishati,” alifafanua Dk Meru.
Alitaja
maeneo mengine kama utafiti wa gesi na mafuta, utoaji wa huduma kwa kampuni za
utafutaji mafuta na gesi katika Bahari ya Hindi.
Kongamano
hilo lilihudhuriwa na watu zaidi ya 400 na wafanyabiashara wa Tanzania walikutana
na wenzao wa Marekani na kuzungumza biashara.
No comments:
Post a Comment