Serikali imesaini makubaliano na Marekani
kwa ajili ya kutekeleza mpango wa nchi hiyo kusaidia maendeleo katika Sekta ya
Umeme.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na Balozi wa
Marekani nchini, Mark Childress walisaini Makubaliano ya Awali juzi
katika Ubalozi wa Tanzania Washington DC, Marekani.
Mpango huo wa Marekani kwa ajili ya
kusaidia maendeleo ya Sekta ya Umeme Afrika ujulikanao kama ‘Power Africa
Initiative’, umetengewa Dola za Marekani bilioni saba na serikali ya nchi hiyo.
Kampuni binafsi za nchi hiyo ziliahidi
kuwekeza Dola za Marekani bilioni tisa 9.
Mpango huo uliozinduliwa na Rais Barack
Obama wa Marekani alipotembelea nchini
Julai mwaka jana. Utainufaisha Tanzania pamoja na nchi nyingine zikiwemo Ethiopia, Ghana, Nigeria, Liberia na Kenya.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini
Marekani, Liberata Mulamula.
No comments:
Post a Comment