Mwenyekiti wa muda Bunge la Katiba, Pandu Kificho akiingia bungeni. |
Rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekingiwa kifua baada ya baadhi ya wabunge wa Bunge Maalumu la Katiba kuunda umoja wa kuitetea na kudhibiti isichakachuliwe.
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao kwa mujibu wa mmoja wa wajumbe wake, Profesa Ibrahim Lipumba, umeundwa mjini hapa kuhakikisha kuwa Rasimu hiyo haichakachuliwi kwa misimamo ya vyama au makundi.
Katika mkutano na waandishi wa habari jana mjini hapa, Profesa Lipumba alisema umoja huo ni wa kila mtu anayekubaliana na mawazo ya wananchi kama yalivyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kupata Rasimu hiyo.
Profesa alisema, katika utoaji maoni kwenye Tume, kulikuwa na uhuru wa kila mwananchi kuchangia kwa njia tofauti ikiwamo kupitia mikutano ya hadhara, barua pepe na simu.
“Isitoshe ile Tume, ilikuwa na watu wazito wa nchi hii wa chama tawala waliokaa na Nyerere (Baba wa Taifa, Mwalimu Julius) kwa muda mrefu. Huwezi kuwa na wasiwasi nao,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema Uwaka haijali chama au kikundi bali inalotaka ni kuheshimu mawazo ya wananchi yaliyo kwenye Rasimu ya Katiba.
“Uwaka si chama kimoja wala umoja wa vyama vya upinzani, bali ni umoja wa wajumbe wote,” alisisitiza.
Alipoulizwa kama msimamo wa Uwaka ni Rasimu hiyo kutochakachuliwa, ni nini maana ya wajumbe kuwamo kwenye Bunge Maalumu la Katiba; Profesa alisema wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wana haki ya kuboresha na kurekebisha na si kuiandika upya.
Alisema Rasimu hiyo ni mwongozo ambao Uwaka inasisitiza umetokana na wananchi na kufafanua kwamba Tume ilifanya kazi kwa miezi 20 wakati wao wana siku 70, ambazo kwa mujibu wake, hawawezi kuandika upya
Katiba.
Alisema, “lakini mwongozo wetu ni ile kazi iliyofanywa na watu kwa miezi 20 wakiwa na Sekretarieti. Sisi tukiwa na siku 70 na watu 629 hatuwezi kusema tunataka Rasimu ya Katiba mpya.”
“Mtu asije akasema hapa ataanzisha mchakato kuandika upya … sisi msingi wetu ni kuhakikisha hivi vifungu havigongani,” alisisitiza Profesa Lipumba.
Akielezea msukumo wa kuanzisha Uwaka, Profesa alisema ni baada ya kujitokeza kauli za baadhi ya watu wanaodai Bunge la Katiba linaweza kuja na mawazo tofauti na ya Tume ya Jaji Warioba.
Vile vile alisema zipo taarifa za kuwapo waraka wa kikundi fulani unaolenga kubadili Rasimu hiyo. “Sisi ndipo tukashituka…ndipo tukasema lazima tuwe na umoja utakaoenzi mawazo ya wananchi,” alisema.
Kwa mujibu wa Profesa Lipumba aliyefuatana na baadhi ya wajumbe wa umoja huo, akiwamo James Mbatia na Profesa Abdallah Safari, idadi ya wanaumoja inakadiriwa kuwa zaidi ya 200.
Alisema wakiwa katika hatua za awali za kuimarisha umoja huo, katika mkutano wa mwisho juzi, idadi yao ilikuwa 120 huku wakitarajiwa kuongezeka.
Ingawa hawajachagua viongozi, Profesa Lipumba ambaye ni mjumbe, alisema wameteua kamati ya kuwashauri inayoongozwa na Profesa Safari. Mkutano mkuu wa Uwaka unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Kura ya siri ya umoja huo kupitia kwa wajumbe hao waliozungumza na waandishi wa habari jana, ulisisitiza kuunga mkono kura ya siri katika uamuzi wa masuala ndani ya Bunge Maalumu.
Profesa Lipumba alisema kura ya siri italinda wajumbe wote wasije kushughulikiwa na taasisi wanazotoka.
Alisema kwa kuwa wanaotaka kura ya wazi hawawezi kukwazika kwa namna yoyote kwa kupiga ya siri, ni vema kanuni ilinde wanaotaka kura ya siri kwa kuwa watakwazika iwapo itatumika ya wazi.
Alisema hoja zinazojengwa kwamba kura ya siri ni maalumu kwa uchaguzi wa mtu na si kwa masuala kama hayo, hazina mashiko kwa kuwa hata Rasimu ya Tatu ya Katiba itapigiwa kura ya siri na wananchi.
Kwa upande wake, Mbatia ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa pamoja na Profesa Lipumba, walisema dhana ya kutishwa na kushughulikiwa ndani ya vyama kwa kwenda kinyume na matakwa, si nadharia.
Alitoa mfano wa kikundi kilichounda G 55 mwaka 1993/94 na pia msimamo wa Mzee Aboud Jumbe wa kutaka serikali tatu, kuwa wahusika waliponzwa na kushughulikiwa ndani ya chama.
Mbatia alisema umefikia wakati ndani ya Bunge Maalumu la Katiba, wajumbe hawaaminiani.
Alisema upo wasiwasi miongoni mwao kwa kuwa kila mjumbe anayetoa mawazo, yapo maswali yanayohoji kuna nini nyuma ya pazia. “Tunaomba tusahau malumbano yetu. Hili si Bunge la Jamhuri. Uvyamavyama bado upo,” alisema.
Katika Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, suala la muundo wa Muungano ndilo limeibua mjadala mkubwa huku likitajwa kuwa kiini cha mgawanyiko katika Bunge Maalumu la Katiba.
Wakati Rasimu ikipendekeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iwe na muundo wa shirikisho lenye serikali tatu, lipo kundi ambalo lina mawazo ya muundo wa sasa wa serikali mbili uendelee.
Serikali zilizopendekezwa kwenye Rasimu ya Katiba ni ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Tanganyika.
Msimamo huo juu ya aina ya muundo wa serikali, ndio unaosadikiwa pia kusababisha msuguano katika upitishaji wa aina ya kura.

No comments:
Post a Comment