Tume ya Mabadiliko ya imeendelea kusikiliza maoni ya makundi maalumu kwa kukutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande na Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Juzi Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph Warioba alisikiliza maoni ya Maalim Seif Sharif Hamad nyumbani kwake Mazizini Zanzibar na jana akasikiliza maoni ya Jaji Chande katika ofisi za Tume ambapo Spika Makinda alisikilizwa katika ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Wakati Chande na Makinda wakiwakilisha makundi ya Mahakama na Bunge, Maalim Seif alisema alikuwa akitoa maoni yake binafsi yasiyofungamana na Serikali wala chama chake cha CUF.
Kama ilivyotarajiwa na wengi, Maalim Seif akiwaelezea waandishi wa habari kuwa anashikilia msimamo wake wa kuwa na Muungano wa Mkataba, huku akiuponda wa sasa wa Serikali mbili kuwa ulipitwa na wakati na usio na tija.
Alisema kwa zaidi ya miaka 49 sasa, Jamhuri ya Muungano iko kwenye mfumo wa Muungano wa serikali mbili huku zikiibuka kero ambazo zimeshindwa kupatiwa ufumbuzi.
Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeunda jumla ya tume 13 za kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano ikiunda tume nane.
“Muungano wa mkataba ndiyo njia sahihi ya kurudisha Muungano utakaokuwa na maslahi…mimi siamini sera ya serikali mbili au tatu, huku kila upande ukiunda tume, lakini hakuna kinachofanyika,” alisema.
Aliongeza kuwa Wazanzibari wamechoshwa na kauli na taarifa za viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakisimama majukwaani kusema muungano unaendelea vizuri.
Maalim alisema kauli hizo zinaathiri maendeleo ya SMZ na watu wake, katika masuala ya Muungano kutokana na kero nyingi zisizo na ufumbuzi.
“Koti la Muungano lililopo sasa kama linakubana sana, ipo haja ya kushona lingine litakalokwenda na wakati wa mabadiliko ya wananchi... sasa tunataka mabadiliko ya Muungano,” alisema Maalim.
Akitetea muundo wa Muungano wa Mkataba, alisema hauna nia ya kuvunja Muungano kwani upo kwa ajili ya kuweka uwazi wa Serikali ya Tanganyika na SMZ.
Alisema muundo wa Muungano huo utakuwa wazi na utaweka bayana mambo yanayofaa kuwa ya Muungano kwa kuwapo ridhaa za pande mbili.
Akifafanua, alitaja mambo ambayo anapendekeza yawe katika muundo wa Muungano wa Mkataba likiwamo suala la ulinzi ambalo alisema ni muhimu kwa Zanzibar.
“Tafsiri ya Muungano wa Mkataba ni kwamba yapo mambo ambayo tutakubaliana kuwa kwenye muundo mpya wa Muungano...hili suala la ulinzi na ushirikiano, tunalihitaji sana,” alisema Maalim.
Lakini akasema hivi sasa makubaliano ya mkataba wa Muungano yamekuwa yanakiukwa kupitia vifungu mbali mbali tangu kifungu cha nne ambacho kinataja mambo 11 ya orodha ya Muungano.
“Hivi sasa mambo yaliyo kwenye orodha ya Muungano ni 22 kutoka 11 ya asili, lakini kwa tafsiri zaidi yamefikia 27 ambayo yameingizwa kinyemela bila ridhaa ya Zanzibar,” alisema.
Alihadharisha kuwa maoni aliyotoa ni yake binafsi na hayafungamani na chama chake cha CUF ambacho yeye ni Katibu Mkuu wake.
Akihutubia Taifa katika uwanja wa Amaan siku ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais Dk Ali Mohamed Shein alisema mafanikio makubwa yamepatikana katika kipindi cha miaka 49 ya Muungano ambao umekuwa na tija na faida kwa pande mbili za Bara na Zanzibar.
Spika Makinda kwa niaba ya Bunge, alisema angependa kuona Tanzania inakuwa na Katiba ambayo itatamka kuwa Spika asitokane na vyama vya siasa na pia asiwe mbunge.
Alisema Spika asiye mwanasiasa atakuwa na fursa ya kufanya uamuzi kwa maslahi ya mhimili huo tofauti na sasa ambapo analazimika atokane na chama cha siasa.
Katiba ya sasa inatoa fursa ya watu wasio wabunge kugombea uspika; lakini lazima atokane na chama cha siasa, jambo ambalo Makinda alisema mfumo huo kwenye Katiba mpya ni vema ukabadilishwa.
Aliongeza kuwa Spika akiwa mbunge inamfanya awe na shughuli nyingi jimboni, kwenye mikutano nje ya nchi, lakini akasema iwapo atakuwa mbunge huru, atajikita zaidi kulitumikia Bunge badala ya jimbo.
Pia alipendekeza mawaziri wasitokane na wabunge ili wafanye kazi kwa usawa kwani mfumo wa sasa unamfanya waziri afanye kazi kwa upendeleo wa jimbo lake, lakini kama waziri atakuwa si mbunge, atafanya kazi bila upendeleo.
Pia alisema kwa kuwa shughuli za Bunge ni nyingi ni vyema ofisi ya Bunge iwe na naibu makatibu wakuu wawili ambao watamsaidia Katibu katika shughuli mbalimbali.
Makinda pia alisema angependa kuona katika Katiba mpya Tanzania inakuwa na mabunge mawili, la wananchi na la Seneti.
Alisema Seneti itakuwa chombo cha kujadili na kupitisha mambo muhimu ya kitaifa ambayo kwa sasa yanakwama kupita katika Bunge lililopo kwa vile wabunge wametanguliza ushabiki wa vyama
vyao.
Jaji Mkuu Chande kwa niaba ya Mahakama, alipendekeza Katiba mpya itamke kuwa Mahakama si chombo cha siasa na ilinde kwa nguvu zote mhimili huo ili uendelee na msimamo wa kutofungamana na upande wowote.
Alisema licha ya kuwa Mahakama kwa sasa iko huru, lakini wao wangependa kuona Katiba inaipa nguvu zaidi ili nchi isiwe na Mahakama ya siasa kwani kufanya hivyo kutavuruga amani.
Kuhusu uteuzi wa majaji, Jaji Chande alisema wangependa kuona unaendelea kufanywa na Rais lakini azingatie ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.
“Tungependa kuona mapendekezo ya Tume ndiyo yanatangazwa na Rais, na asiingize jina kutoka sehemu nyingine na asishauriane na Tume hiyo ikiwa imetoa mapendekezo yake,” alisema Jaji Mkuu.
Alipendekeza Tume hiyo iboreshwe kwa kuongezwa wajumbe kutoka sita wa sasa hadi 12. Wa sasa ni Jaji Mkuu, Jaji Kiongozi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wajumbe wawili wa kuteuliwa na Rais na Jaji wa Mahakama ya Rufaa.
Alisisitiza nchi itawaliwe na Katiba badala ya Serikali, Bunge au Mahakama. Alisema iwapo Katiba itaongoza nchi kutakuwa na kuheshimiana kati ya mihimili iliyopo na pia suala la utawala bora litaboreka.
Taarifa kutoka ndani ya Tujmem, zilieleza kuwa mwingine aliyepata fursa jana ya kutoa maoni ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, hata hivyo haikueleza alitoa maoni juu ya nini.

No comments:
Post a Comment