Aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani ambaye kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba mjini hapa, amepandishwa kizimbani akidaiwa kufumaniwa na mume wa mtu.
Katika shauri hilo katika Mahakama ya Mwanzo mjini hapa mbele ya Hakimu Meddy Mkinga, mlalamikaji Asteria Mgabo anamtaka Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa.
Hata hivyo, mtawa huyo alionekana kutotulia sehemu moja katika eneo hilo la Mahakama na alitoweka ghafla kesi ilipotajwa mahakamani hapo.
Katika hati ya madai inadaiwa kuwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe ambaye jina halijafahamika wakiwa chumbani kwenye nyumba ya kulala wageni ya Chipu iliyoko eneo la Katandala mjini Sumbawanga.
Hakimu Mkinga alipotaja kesi hiyo, mdaiwa hakutokea kwenye chumba cha Mahakama ikamlazimu aiahirishe hadi Januari 21 na mshitakiwa yuko nje kwa kuwa shauri hilo la madai halina masharti ya dhamana.
Baadhi ya watawa wa kike ambao hawakuwa tayari majina yao yaandikwe walikiri kumfahamu mlalamikiwa kwamba alikuwa mtawa wa Shirika la Masista wa Maria Mtakatifu Malkia wa Afrika (MMMA) ambapo wanadai aliachana na maisha ya utawa kwa hiyari yake miaka miwili iliyopita.
“Sisi tutamwombea mwenzetu huyo kwa sala … tuliishi naye lakini aliamua tena bila shuruti kuachana na maisha haya ya utawa … aliaga na kuomba apumzike kwa miezi kadhaa uraiani ili ajifikirie kurejea au kuachana na maisha haya.
“Sisi kama watu wazima, tulimwelewa anamaanisha nini sasa ndiyo haya yamemkuta, tutaendelea kumwombea katika sala zetu za kila siku,“ alisema mmoja wao.
Yasinta ambaye ni mhudumu wa afya katika hospitali ya mkoa wa Rukwa mjini hapa amekuwa gumzo karibu kila kona mjini hapa kutokana na shauri linalomkabili mahakamani.

No comments:
Post a Comment