Naibu Waziri Aggrey Mwanri. |
Kufuatia Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri kuwa mkali na kukagua ujenzi wa miradi ya kijamii mkoani Rukwa kwa umakini mkubwa na kubaini mapungufu mengi mkewe Agnes Mwanri amefunguka na kusema ndivyo alivyo hata akiwa nyumbani kwao .
Mama Mwanri ambaye anafuatana na mumewe katika ziara ya kikazi ya siku sita mkoani hapa ambapo tayari ameshatembelea na kukagua ujenzi wa maendeleo katika Halmashauri za Kilambo, Sumbawanga na Manispaa ya Sumbawanga alifunguka na kusema hayo juzi wakati alipokuwa akiwasalimia wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji Wipanga katika Manispaa ya Sumbawanga .
Alisema; “msimshangaye mkadhani anajipendekeza hapana yeye (Mwanri) ndiyo alivyo hata akiwa nyumba nafanya vitu vyake kwa umakini wa hali ya juu na hapendi kudanganywa wala kuona watu wakidhulumia haki zao
“Mume wangu ndivyo alivyo hata akiwa nyumbani kwanza hapendi uonevu wala udanganyifu wa aina yeyote ile yeye siku zote anasimama katika haki… Hivyo nimeamua kuwaeleza haya kwa sababu kutokana na kuwa makini katika kazi zake hususani anapokagua ujenzi wa miradi, isieleweke kuwa anajipendekeza la hasha yeye ndivyo alivyo,” alisema.
Mwanri amekuwa kivutio kikubwa na kumwagia sifa kemkem na wananchi katika maeneo mbalimbali alipotembelea na kukagua ujenzi wa miradi ya kijamii wakidai kwamba hawajawahi kushuhudia kiongozi yeyote wa ngazi za juu akikagua ujenzi wa miradi hiyo kwa umakini wa hali ya juu .
“Sisi tunasema ameonesha njia basi na viongozi wetu waige mfano wake uliotukuka hatujawahi kushuhudia umakini wake Naibu Waziri huyu hasa anapokagua ujenzi wa miradi ya kijimii yaani anafahamu mambo mengi ya kiufundi kuliko hata wahandisi wenyewe.
“Tunamfananisha na John Magufuli (Waziri wa Ujenzi) na Harrison Mwakyembe (Waziri wa Uchukuzi) kwa hakika hawa watatu ni majembe hatuna ubishi nao,” alisena John Ngweshi kijijini Wipanga .
Lakini licha ya umakini wake pia wengi wameguswa na uwezo wake wa kuongea katika mikutano ya hadhara na ya ndani kwa zaidi ya saa sita mfululizo bila kupumzika.
Juzi Naibu Waziri huyo alikuwa kivutio kikubwa mjini Sumbawanga pale alipotembea kwa miguu kwa zaidi ya saa moja akikagua miradi ya ujenzi wa barabara mjini humo iliyojengwa kwa kiwango cha lami na Stendi Kuu ya mabasi.
Kutokana na umakini wake huo Mwanri ameweza kubaini mapungufu mengi ya ujenzi katika miradi mbalimbali ikiwemo ya vyumba vya madarasa, barabara, majengo ya miradi muhimu ambayo mengi yamejengwa chini ya kiwango.
Mbali ya kuwa makini hivyo lakini pia anapenda mizaa kwani katika siku ya kwanza ya ziara yake kijijini Tunko alibaini kuwa jina lake kwenye mabango ya matangazo ya kumkaribisha katika Halmashauri ya Sumbawanga lilikuwa limekosewa hivyo alimwagiza Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Moshi Chang’a kulifuta na kuliandika upya.
“Mimi siwezi kunong’ona nimesoma kwenye vitambaa vya matangazo ya kunikaribishwa vilivyotundikwa barabarani jina langu limekosewa sasa kwa sauti kubwa nakuuagiza DC ulirekebishe mara moja kabla sijaondoka hapa,” aliagiza.
Kufuatia agizo hilo ililazimu mawe yote ya msingi aliyopangiwa kuweka au kuzindua yalilazimika kurekebisha herufi ya mwisho ya jina lake la mwisho.
Lakini pia alimshukuru kwa namna ya pekee Mbunge wa Jimbo la Kwela (CCM), Ignas Malocha kwa kumpatia heshima ya kipekee kwa mapokezi aliyomuenzi ikiwemo kumvalia suti na tai za gharama kauli iliyowafanya wengi kuangua kicheko.

No comments:
Post a Comment