Abiria huyo mlevi akiwa amedhibitiwa na wenzake kwa kufungiwa kwenye kiti chake hadi mwisho wa safari. |
Abiria mlevi katika ndege ya New York iliyokuwa ikitokea Iceland alijikuta akifungwa kwa utepe katika kiti chake na abiria wenzake baada ya kumshambulia mwanamke mmoja, kuwachoma abiria wengine kwa chuma chembamba na kupiga mayowe kwamba ndege hiyo ilikuwa ikianguka.
Mmoja wa rafiki wa abiria walioshuhudia, Andy Ellwood wa New York, alituma picha ya mlevi huyo aliyedhibitiwa kwenye mkokoteni wake ukiwa unahusiana na tukio hilo.
"Abiria huyo alikunywa pombe zake zote za bure katika ndege kutoka Iceland hadi uwanja wa ndege wa John .F. Kennedy (JFK) wiki iliyopita," aliandika Ellywood.
"Alipofikia hatua ya kutodhibitika, (kama kujaribu kumkaba mwanamke aliyekaa pembene yake na kuanza kupiga mayowe kwamba ndege inaelekea kuanguka), abiria wenzake walimdhibiti na kumfunga kwenye kiti chake kwa umbali wote uliobakia katika safari ya ndege hiyo. Alisindikizwa na polisi kutoka ndani mara ndege hiyo ilipotua."
Picha hiyo ilitumwa kwa Ellwood sababu yeye na rafiki yake walipendelea kufanya biashara ya 'simulizi za safari za kivita' alisema.
Rafiki yake ambaye alishuhudia mkasa wote katika ndege hiyo hakutaka kujitambulisha au kuongea na vyombo vya habari.
Mtu huyo mwenye miaka 46, ambaye jina lake halikuwekwa hadharani, alikamatwa mara baada ya kutua kwenye uwanja wa JFK Alhamisi iliyopita.
Alikutwa na pasi ya kusafiria ya Iceland, kwa mujibu wa Msemaji wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege, Ron Marsico.
Kashikashi za abiria huyo zilianza baada ya masaa kadhaa angani pale yalipobaki takribani masaa mawili kufikia mwisho wa safari, liliripoti jarida la habari la Iceland la Mbl.is.
Makamu wa Rais wa Mawasiliano wa Shirika la Ndege la Iceland, Guðjón Arngrímsson, aliwathibitishia waandishi wa habari kwamba mtu huyo alikuwa akihatarisha amani, lakini hakuzungumzia chochote kuhusu picha hiyo.
Abiria huyo asiyedhibitika alipelekwa hospitali huko Queens baada ya kuwa ameshushwa kutoka katika ndege hiyo, alisema Marsico wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege.
Waendesha mashitaka walikataa kumfungulia mashitaka kwa kile alichofanya sababu abiria wengi walikuwa kimya kuzungumzia vurugu zake kwa mamlaka, gazeti la New York Post liliripoti.
Katika tukio linalofanana na hilo, polisi walimkamata rubani wa American Eagle baada ya kushindwa kipimo cha kilevi kwenye damu kabla ya kuwa amepangiwa kurusha ndege kutoka Minneapolis kwenda New York, Alhamisi ya wiki iliyopita.
Kolbjorn Jarle Kristiansen alikuwa akijiandaa kwa ukaguzi kabla ya kurusha ndege majira ya Saa 12:30 asubuhi pale polisi, baada ya kutonywa, kuvamia ndege hiyo na kumfanyia kipimo hicho cha kutambua kilevi.
Alikamatwa kwa tuhuma za kuwa amelewa pombe.
Abiria walikuwa bado hawajaingia kwenye ndege hiyo, ambayo ilichelewa kwa masaa mawili na nusu wakati rubani mbala alipopatikana, kwa mujibu wa Matt Miller, msemaji wa shirika dada la ndege, American Airlines.
Kristiansen amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi.

No comments:
Post a Comment