Dk Khoti Kamanga. |
Viongozi wa dini ya Kiislamu wanaohudhuria warsha ya kuzuia mauaji ya kimbari, wameweka bayana kuwa uamuzi wa Serikali kugoma kuanzisha Mahakama ya Kadhi na kuwaachia Waislamu wenyewe, unawakera na unaweza kuchangia uvunjifu wa amani nchini.
Wamesema Waislamu kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuanzishwa kwa mahakama hiyo, lakini kwa kile kilichodaiwa kuwa mashikizo ya dini zingine, yamesababisha Serikali kugoma kuianzisha na kuigharimia mahakama hiyo.
Viongozi hao walitoa michango hiyo baada ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Khoti Kamanga kutoa mada kuhusu viongozi wa dini na mauaji ya kimbari katika warsha inayoendelea Dar es Salaam.
“Waislamu wanadai Mahakama ya Kadhi, Serikali imegoma, huoni kama hivi ni viashiria vinavyoweza kuvuruga amani ya nchi na hata kusababisha mauaji ya kimbari kama ilivyotokea kwa nchi zingine?” Alihoji Shekhe Salim Barayaini kutoka Tanga.
Naye Shekhe Hassan Yabeki kutoka Mwanza, alitaja mambo yanayoweza kusababisha migogoro ya kidini hapa nchini kuwa ni pamoja na hospitali za madhehebu ya Kikristo kuwavalisha wagonjwa wanaolazwa kwenye hospitali hizo mavazi yenye nembo ya msalaba.
Alisema hospitali hizo licha ya kuwa ni za madhehebu ya dini, lakini hugharamiwa sehemu ya fedha ambazo ni za walipa kodi wote bila kujali itikadi zao na Serikali.
“Kwa hali hii kwa nini mgonjwa alazimishe kuvalishwa mavazi yenye nembo ya msalaba? Alama hii kwa Mkristo ina maana ya ushindi, lakini kwa Mwislamu ina maana tofauti,” alisema Shekhe huyo.
Alilalamika kuwa suala hilo haliishii kwa wagonjwa tu, bali hata mtu anayeenda kumwona mgonjwa anapewa beji yenye alama ya nyoka jambo ambalo alisema pia linawakera Waislamu.
Kiongozi huyo alisema kuna mkakati wa madhehebu ya Kikristo kutaka kuteka imani za watu wengine na akatoa mfano kuwa ukienda katika hoteli mbalimbali hapa nchini, chumbani ni lazima kutakuwa na kitabu cha Biblia peke yake.
“Korani huikuti, je huu si mkakati wa kuweka imani za watu wengine? Alihoji Shekhe huyo na kutolea pia mfano wa kwenye mabasi ya abiria kuwa dereva anajiamulia kuweka nyimbo za dini bila kujali tofauti za imani za abiria wake.
Katika mada yake, Dk Kamanga aliwaonesha namna viongozi wa dini walivyoshiriki kwenye mauaji ya kimbari kweye nchi za Yugoslavia, Serbia na Rwanda na kwamba hali hiyo inaweza pia kujitokeza nchini kama viogozi hao hawatakuwa na uadilifu.
Dk Kamanga aliwaeleza viongozi hao kuwa ili kuepusha taifa na uwezekano wa kuingia kwenye machafuko yanayoweza kusababisha mauaji ya kimbari ni lazima wasisitize thamani ya uhai wa mtu.
Pia aliwataka viongozi hao kujenga utamaduni wa kuwa na uungwana na kutovumilia vitendo vyovyote vya ubaguzi; watambue kuwepo kwa imani tofauti za kidini na kuvumiliana na kujenga mawasiliano kati ya dini moja na dini nyingine.
Dk Kamanga pia alitaka Serikali itekeleze jukumu lake la kuzuia mauaji ya kimbari na kuweka sheria ya mambo hayo.
“Kwa sasa hatuna sheria ya mauaji ya kimbari, likitokea la kutokea leo hii sheria ya namna hiyo haipo, itakuwa kazi, ni vyema Serikali iingize suala hilo kwenye sheria zetu za makosa ya jinai,” alisema Dk Kamanga.
Pia alisema kwa kuwa nchi iko kwenye mchakato wa kutunga Katiba mpya, Katiba hiyo itoe fursa za uhuru wa kuabudu na kuvumiliana ili kulinda amani na utulivu uliopo kwa sasa.

No comments:
Post a Comment