MAMA ALIYEMPA KIPIGO MWANAE AKIONA CHAMOTO GEREZANI...

Mama mwathirika kiakili aliyefungwa kwa kumpa kipigo kikali mtoto wake wa kiume amepigwa na wafungwa wenzake wakilipiza visasi dhidi yake.
Wenzake katika jela ya wanawake pekee walimwangushia adhabu ya kipigo mwanamke huyao mwenye miaka 29 baada ya kumvurumishia makombora, mahakama ilielezwa.
Katie Burston, mwenye miaka 26, alikuwa ni miongoni mwa kundi lililomzingira Bi Biggs na mfungwa mwingine ambaye si maarufu wakati wawili hao wakijikunyata ndani ya banda wakirusha makombora.
Bi Biggs amefungwa mwaka 2009 akitumikia kifungo cha miaka nane kwa kumfanyia ukatili mtoto baada ya kifo cha mwanae wa kiume aliyekuwa na umri wa wiki nane tu aliyevunjika mbavu zake, bega na kifundo cha mkono.
Katika kesi hiyo ambayo imekumbushia tukio la kesi ya Baby P, mwathirika wa dawa za kulevya na rafiki yake wa kiume mwenye kesi za ubakaji waliruhusiwa kumtunza mtoto Rhys Biggs, japo Biggs alikuwa na mtoto wake wa kwanza ambaye alinyang'anywa sababu ya tabia yake ya kupindukia katika dawa za kulevya.
Biggs alikimbizwa hospitali huku akichuruzika damu katika jeraha kichwani mwake na damu iliyovilia mwilini mwake baada ya kuwa ameshambuliwa kwa kutumia chuma katika bustani ya HMP Send karibu na Woking, huko Surrey.
Burston wa Paignton, Devon, alihukumiwa baada ya kukiri makosa katika siku za mwanzo za usikilizwaji wa kesi hiyo kwa ugomvi uliosababisha kudhuru mwili.
Mahakama ya Guildford ilielezwa kwamba Bi Biggs, ambaye sasa ana miaka 30, anayeishi Newham, East London alikuwa akichukiwa na wenzake sababu ya makosa yake dhidi ya mwanae wa kiume mwenye wiki nane.
Robin Sellers, akiendesha mashitaka, alisema: "Bi Biggs hakuwa mashuhuri gerezani humo sababu ya aina ya hatia yake."
Siku ya shambulio hilo, Julai 31, mwaka jana yeye na mwenzake asiyekubalika, Dawn Gregory wakipangiwa kazi kwenye bustani, mbali na ghadhabu ya wafungwa wengine.
Sellers alisema kwamba wakati wakitekeleza majukumu yao, Bi Biggs na Dawn walitakiwa kwenda kwenye banda - lakini wakajikuta wakishindwa kutoka nje baada ya kuzingirwa na wafungwa wengine.
"Banda hilo liliharibiwa kwa kushambuliwa kwa mawe," alisema.
Kisha kundi la wafungwa waliobeba zana za kutengenezea bustani likawavamia waathirika hao wawili.
Bi Biggs alishambuliwa kwa mpira wa maji na kipande cha ubao," alisema Sellers.
Mahakama ilielezwa kwamba Bi Biggs alipelekwa hospitali baada ya kupata mpasuko wenye urefu wa takribani sentimeta tano usoni pamoja na kuvilia damu kisogoni na sehemu nyingine mwilini mwake.
Katika taarifa ya madhara ya mwathirika, mwanamke huyo aliyejeruhiwa alisema: "Majeraha yangu yalichukua wiki kutibika."
Bi Biggs alisema amekuwa akihisi fadhaa na kwamba analazimika kusindikizwa popote aendako na mfungwa ambaye ni rafiki yake ama ofisa wa gereza.
Mahakama ilielezwa kwamba wakati wa shambulio hilo mwathirika huyo wa zamani wa dawa za kulevya Burston alikuwa akitumikia kifungo cha miaka miwili na miezi minane jela baada ya kupatikana na hatia ya uporaji na kujaribu kupora huko Exeter.
Alifungwa mwaka 2010 na Makahama ya Exeter kwa kumpiga mwanaume mlemavu mwenye miaka 73, kumfungia kwenye kiti chake cha magurudumu nyumbani kwake huko Exeter, na kuiba funguo zake Agosti 14, 2010 - baada ya kushindikana jaribio lake la kumpora siku mbili kabla.
Wakili wa utetezi, Jeremy Sharples alisema mteja wake sasa ameachiwa kwa leseni kutoka kifungoni na ameachana na dawa za kulevya.
Alisema ana mtoto wa kiume mwenye miaka saba na alikuwa akimwongoza kwenye maisha yaliyonyooka - akijaribu kuachana na matukio ya nyuma.

No comments: