MADADA WAWILI NDUGU WAFA KWA AJALI YA GARI MAPUMZIKONI MOROCCO...

KUTOKA JUU: Pippa, Tara na Joshua. KULIA: Mji wa Rabat ambako ajali iliyochukua uhai wa madada hao ilitokea.
Madada wawili wamekufa katika ajali ya gari nchini Morocco wakati wakiwa kwenye 'ziara ya aina yake maishani'.
Tara Darlington mwenye miaka 23, na dada yake Pippa mwenye miaka 21, ambao walielezewa na wazazi wao kuwa ni marafiki wakubwa, walikufa baada ya gari lao la kukodi kugongana na gari lingine mapema asubuhi ya Jumatatu.
Rafiki yao, Joshua Stump mwenye miaka 21, alijeruhiwa vibaya na yuko mahututi hospitalini, polisi walisema juzi.
Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Rabat ulioko kaskazini-magharibi wakati wa mapumziko kabla ya madada hao kuanza mwaka wao wa mwisho chuo kikuu.
Walikuwa wakisafiri sehemu mbalimbali Afrika na walikuwa Mauritania wiki mbili zilizopita.
Wazazi wa madada hao, Patrick na Emma Darlington walisema juzi: "Sisi kama familia tumehuzunishwa mno kwa kuwapoteza mabinti zetu wote, Tara na Pippa.
"Walikuwa warembo sana, wachapakazi na wenye upendo ambao walileta nuru na ucheshi kwa yeyote aliyekutana nao.
"Waliweka utofauti katika maisha mengi mbalimbali na waliangazia katika kila chumba walimoingia. Safari hii ilikuwa ni ziara za aina yake kwao maishani ambayo waliipanga, kufanya kazi kwa bidii na kuwekeza fedha kwa pamoja kwa miezi kadhaa.
"Waliungana katika ziara hii na Josh Stump ambaye yuko mahututi akipigania roho yake katika hospitali ya Rabat. Mawazo yetu na sala tumevielekeza kwake na wazazi wake pamoja na mdogo wake, Emily." Madada hao walikuwa wenyeji wa Whiteparish, karibu na Salisbury, Wiltshire. Joshua anatokea Salisbury.
Patrick mwenye miaka 62, Mkurugenzi katika kampuni ya yellow Bike, na mkewe, Emma mwenye miaka 52 ambaye ni kocha, waliongeza kwamba Tara na Pippa walikuwa ni marafiki wakubwa 'ambao walipenda kufanya kila kitu kwa pamoja'.
Waliendelea: "Mapacha hao wa Darlington' walitegemeana sana". Walikuwa wakitumia muda wao wa furaha maishani na kuahidi kurejea nyumbani baada ya siku kumi.
"Tara na Pippa walikuwa kila kitu kwao wenyewe na kwetu pia. Tutawakumbuka daima. Wataendelea milele kuwa vijana na pamoja."
Kaka wa madada hao, Oscar mwenye miaka 15 alisema: "Ni madada zangu wapenzi na nawapenda mno.
"Nilikuwa nakaribia rika ambalo tungeweza kufanya vitu mbalimbali pamoja. Wametoweka mapema lakini hawawezi kusahaulika na kila wakati kwenye moyo wangu." Tara alikuwa akisomea utangazaji, uandishi wa habari na elimu-jamii huko Goldsmiths, Chuo Kikuu cha London, na alishaanzisha Savvy Social Media, taasisi yake ndogo, inayotoa huduma kwa wafanyabiashara wadogo.
Pia alikuwa akifanya kazi katika mtandao wa Spashion.com, jarida la mtandaoni kuhusu michezo na mitindo. Alishakabidhiwa majukumu mjini New York kuyashughulikia baada ya kumaliza chuo kikuu.
Pippa yeye alikuwa akisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Newcastle.

3 comments:

Anonymous said...

zorgverzekering vergoeding vergelijk studentenzorgverzekering
zorgverzekering voor studenten vergelijken goedkope jongerenverzekering
My weblog : studenten zorgverzekeringen

Anonymous said...

utrecht verhuizen
My web page: bert ooms verhuizingen

Anonymous said...

Tremendous issues here. I'm very happy to peer your article. Thank you a lot and I am taking a look ahead to touch you. Will you please drop me a e-mail?

Here is my site :: twitter supplier