KUSHOTO NA KULIA: Mtu huyo ukiwa umetelekezwa chini baada ya kuchomwa moto na watu wenye hasira. JUU: Mama wa Julio Saquil akiwa mbele ya kaburi la mwanae. CHINI: Mwanamke mmoja akipita kando ya damu zilizosalia baada ya kuondolewa mwili wa Julio.
Kundi la memba wa kamati ya wazalendo huko Guatemala limefanya malipizi ya kutisha dhidi ya mtu ambaye mamlaka husika zimesema aliua watoto wawili katika shule moja ya msingi.Waziri wa Mambo ya Ndani nchini humo, Mauricio Lopez Bonilla alisema Julio Saquil huku akiwa amelewa aliingia katika shule hiyo iliyopo kwenye jimbo la kaskazini la Alta Verapaz juzi na kuwakata kooni watoto wawili kwa kutumia panga.
Bonilla alisema baada ya hapo kundi hilo lilimchoma moto mtu huyo mwenye miaka 35 katika eneo la shule hiyo na aliungua hadi kufa.
"Aliingia katika moja ya madarasa na kuwashambulia wanafunzi, kumkata kabisa kichwa mvulana wa miaka 13 na kumchana kooni binti wa miaka minane kwa kutumia panga," askari zimamoto Wilson Cahuec alisema.
Maofisa usalama walisema mtu huyo aliyeuawa ana historia ya matatizo ya dawa za kulevya na ghasia, lakini hawakueleza sababu za yeye kufanya shambulio hilo kwa watoto hao.
Imeripotiwa kuwa kundi hilo liliundwa na mchanganyiko wa walimu na wananchi kadhaa wakazi wa eneo hilo.
Walisema pia kwamba Mamlaka husika zimewataja watoto hao kuwa ni Evelyn Yanisa Saquij Bin mwenye miaka minane na Juan Armando Coy Cal mwenye miaka 13.
Maofisa walisema miili ya watoto hao ilikutwa na majeraha.
Makundi ya mauaji yameshamiri katika maeneo ya Guatemala ambako polisi wako wachache.
Taasisi ya Haki za Binadamu nchini humo imesema majaribio 234 ya mauaji yamefanyika mwaka 2011 na takribani watu 40 waliuawa.
Kufuatia matukio ya kutisha ya vurugu, hofu imetanda katika maeneo jirani, ambao wameanza kujichukulia sheria mikononi kuadhibu wahalifu.
Watu wanne walioshukiwa kuwa wezi walikamatwa na kupigwa na wakazi wenye hasira kali ambao kwa kawaida walidhani njia zao za adhabu zilikuwa mwafaka kwa wasimamia sheria.
Shukrani, angalau kwa watu hao, waliokolewa na polisi na kutiwa mbaroni, lakini tu ni baada kuwa wamekamatwa, kuchapwa kwa fimbo, kudundwa ngumi na kutandikwa mateke.
No comments:
Post a Comment