Mtu mwenye michoro ya tatoo mwili mzima ambaye alikiri kupora majumbani na kuiba magari kwa ajili ya kupata pesa za kununulia dawa za kulevya aina ya heroin, amepandishwa kizimbani kwa kumfyatulia risasi ofisa wa polisi.
Jason Barnum alishitakiwa shitaka moja la kujaribu kuua na mawili ya kushambulia baada ya tukio lililotokea Merrill Field Inn huko Anchorage, mjini Alaska, Alhamisi iliyopita.
Mtu huyo mwenye miaka 37, ambaye sura yake imefunikwa kwa michoro ya mafuvu na mifupa mitupu, midomo yake ikiwa imechorwa meno na jicho lake la kulia likiwa limechorwa weusi, alikuwa akiyumba kutoka upande mmoja hadi mwingine katika mahakama, wakati mwingine akijibamiza uso wake kwenye kipaza sauti.
Polisi wanaamini kuna uwezekano alikuwa katumia dawa za kulevya wakati wa kutupishiana risasi ambako kulifanyika baada ya maofisa kugundua gari lililohusishwa katika wizi likiwa kwenye maegesho ya hoteli muda mrefu, kwa mujibu wa ripoti.
Jason, ambaye alipigwa picha kwenye mtandao wa Facebook, anahusishwa na matukio saba ya uporaji katika eneo la Anchorage Hillside, mengi yakitokea wakati wahusika wakiwa majumbani kwao.
"Unapokwenda kwenye nyumba ya watu usiku, hiyo ni tabia yenye mashaka na hiyo si kawaida ya wezi," alisema Luteni Anthony Henry.
Wakitumia uchunguzi wa nyendo, maofisa waliweza kugundua yuko kwenye chumba namba 209 cha hoteli hiyo ambako walimkuta akiwa na wenzake wawili ambao pia kulikuwa na vibali vyao wakitakiwa kukamatwa.
Polisi walipomfunga pingu mmoja wa jamaa zake, Jason akaanza kuwafyatulia risasi maofisa kwa kutumia bunduki iliyoibwa kwenye nyumba moja aliyofanya uporaji.
Polisi walijibu mashambulizi, na kumjeruhi Jason begani.
Ofisa mmoja alijeruhiwa pale risasi ilipoteleza chini ya fulana yake na kulazimika kushonwa nyuzi chache katika jeraha hilo.
Jason aliungama kuhusika katika matukio takribani matatu ya hivi karibuni, akiongeza kwamba alipora majumbani kwa ajili ya kujipatia fedha kwa ajili ya kumudu kununua dawa za kulevya.
Picha za Facebook zinaonesha michoro ya kutisha ya tatoo ikiwa imetapakaa mwilini mwake, kukiwa na neno 'maumivu' limeandikwa kwenye msuli wa mkono wake wa kulia.

No comments:
Post a Comment