MWANAMKE AVUA NGUO ZOTE UWANJA WA NDEGE KWEUPEEE...

Mwanamke huyo akiwa amesimama mtupu mbele ya maofisa.
Pengine alikuwa akithibitisha kuwa hakuficha chochote ama pengine alidhani maofisa walitaka kukagua mwili wake!
Vyovyote vile ni kwamba ilikuwa kizaazaa kikubwa uwanjani pale mwanamke mmoja alipoamua kuvua nguo zake zote na kubaki mtupu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Denver, juzi asubuhi.
Tukio hilo la kustaajabisha lilitokea majira ya saa 2:45 asubuhi pale mwanamke alipokamatwa akivuta sigara kinyume cha sheria kwenye lango la wasafiri wanaowasili.
Wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege walimwambia mwanamke huyo azime sigara badala yake akawavulia nguo zote.
Akiwa bado kasimama mtupu, mwanamke huyo aliwataka maofisa kumgongea muhuri pasi yake ya kusafiria.
Haikufahamika mara moja kwanini alivua nguo zake lakini polisi wamesema kwamba suala la sigara lilikuwa halihusiki. Waliongeza kuwa aliwaambia maofisa kwamba alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kukosa usingizi.
Msemaji wa polisi Denver, Sonny Jackson alisema: "Inaonekana kuna kutokuelewana."
Aliongeza: "Mwanamke huyo aliwaeleza maofisa kuwa hakupata usingizi usiku wa jana yake."
Shuhuda mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake, alisema abiria karibu wote walibakia kumkodolea macho tu mwanamke huyo.
"Wote tulishitushwa," alisema. "Hakika hakuna aliyemgundua hapo kabla sababu kila mmoja alikuwa akihangaikia kupata ndege yake. Ndipo kila mmoja akabaini kuwa amesimama pale akiwa mtupu kabisa."
Wazazi walikimbia kuwafunika macho watoto wao ili wasimuone mwanamke aliyesimama mtupu. Abiria wengine walionekana wakipita huku wakimkodolea macho.
Baada ya dakika takribani 20 akiwa amesimama mtupu, mwanamke huyo asiyefahamika alipelekwa hospitali kwa uchunguzi. Hakukamatwa na wala hakufunguliwa mashitaka.
Uwanja huo wa ndege una vyumba viwili kwa ajili ya wavutaji sigara. Msemaji wa Uwanja wa Ndege, Laura Coale hakuna eneo la kuvulia nguo na wala hakuna mpango wa kutenga eneo hilo.

No comments: