Binti wa miaka mitano amebakia kuwa na hofu kubwa maishani baada ya kushambuliwa vibaya na mbwa.
Abbie Varrow alikuwa akicheza mchezo wa kuruka juu-chini kwenye kitanda maalumu karibu na uzio wa nyumba jirani ndipo mbwa huyo hatari alipomnasa juu ya uzio na kumshambulia kwa meno makali binti huyo usoni na kumjeruhi vibaya.
Tukio hilo lilidumu kwa sekunde kadhaa lakini iliwachukua madaktari wa upasuaji masaa mawili kushona majeraha kwa nyuzi 60. Mishipa yake ya fahamu puani imeharibika kabisa.
Juzi mama yake, Alyson alisema ilikuwa bahati kwa Abbie na rafiki yake kunusurika kifo.
"Najaribu kufikiri ingekuwaje kama mbwa yule angerukia upande wa pili wa uzio na kuingia ndani," alisema Bi. Varrow mwenye miaka 40.
Shambulio hilo lilitokea wakati Abbie akicheza na rafiki yake Harry Chapman, ambaye anaishi jirani na kwao Breat Notley, Essex.
Bi. Varrow alisema: "Tulisikia Abbie akilia na kisha mmoja kujibamiza kwenye mlango wa mbele."
"Chini ya jicho lake la kushoto akionekana kuchanwa huku nyama ikining'inia na tulishangaa kuona hakunyofolewa jicho. Damu nyingi ilikuwa ikichuruzika kutoka kwenye jeraha."
Aliongeza: "Kitu cha kwanza Abbie alichoulizia akiwa hospitali ni kioo na alipojitazama akasema, "Nimeumia sana, au sio?"
"Hatujui kitakachotokea kwa sasa na ngozi yake itapona kwa kiasi gani lakini tuna mashaka na pua yake. Anaendelea kusema inachekesha."
Shambulio hilo lililotokea Machi 27 lilimwacha Abbie, ambaye wazazi wake wana watoto wengine kumi kwenye mahusiano yao ya awali, akiwa bado amelazwa kwenye Hospitali ya Broomfield mjini Chelmsford kwa siku mbili. Anatarajia kurejeshwa tena hospitalini hapo mwezi ujao.
Baba yake, Tony mwenye miaka 39, muuza duka, aliongeza: "Likikuwa ni tukio shambulio lisilotegemewa.
"Abbie alikuwa ni mtoto asiye na hofu lakini sasa amekuwa mwoga kila aonapo mbwa wakubwa. Ametikiswa mno kwa sasa. Hatumlaumu mbwa lakini kwa zaidi ya asilimia 110 lawama zetu tunazielekeza kwa wamiliki."
"Mpaka sasa hawajafanya lolote tangu pale watoto wao walipokuwa wakishangilia tukio hilo wakipiga kelele "Ua, ua, ua".
"Nataka washitakiwe kwa hili lililotokea."
Mkewe amependekeza kurejeshwa kwa utaratibu za leseni za kumiliki mbwa, ambazo zilisitishwa nchini Uingereza mwaka 1987.
Polisi wa Essex wamesema wamiliki wa mbwa huyo wanashikiliwa kwa tuhuma za kumiliki mbwa hatari.
No comments:
Post a Comment