Baada ya kusikia mgonjwa mmoja kwenye hospitali ya wagonjwa wa akili ameokolewa alipokuwa akijaribu kujiua kwa kujizamisha kwenye kisima, daktari akapitia tena faili la yule mgonjwa aliyemwokoa mwenzake na kumwita ofisini kwake. "Nimepitia faili lako na mwenendo wako unaonesha kwamba umepona hivyo nakuruhusu urudi nyumbani. Lakini jambo la kusikitisha ni kwamba yule jamaa uliyemwokoa amejinyonga kwa kamba kwenye mti na kufa." Ndipo yule kichaa akadakia, "Hajajinyonga dokta, ni mimi nilimtundika ili akauke maji."
No comments:
Post a Comment