MASIKINI! JUMBA LA O.J. SIMPSON HATARINI KUPIGWA BEI...

KUSHOTO: Hekalu la O.J Simpson ambalo liko hatarini kuuzwa. PICHA NDOGO: Arnelle Simpson. KULIA: O.J. Simpson akiwa mahakamani wakati wa kusomewa hukumu yake.
Imefahamika kwamba O.J. Simpson yuko hatarini kupoteza hekalu lake lililoko Florida Kusini kufuatia binti yake mkubwa Arnelle kulimbikiza deni la hekalu hilo kwa miaka miwili sasa.
Kwa mujibu wa Jarida la National Enquirer, Simpson amekasirishwa mno na kumlaani binti yake kwa kufuja fedha zake za pensheni Dola za Kimarekani 25,000 anazolipwa kwa mwezi.
Marejesho ya mkopo wa hekalu lake hilo lenye vyumba vinne vya kulala ni Dola za Kimarekani 3,133 kwa mwezi.
Lakini nyaraka zimebainisha kuwa mkopo huo haujalipwa tangu mwaka 2010 licha ya ukweli kwamba mtuhumiwa huyo alimuamini mno Arnelle kusimamia vipaumbele vyake na mali zake baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 33 jela kwa kosa la utekaji nyara, uporaji wa kutumia silaha na makosa mengine ya udhalilishaji mwaka 2008.
Vyanzo vimelieleza Enquirer: "O.J. alilazimishwa kusaini karatasi kupinga uwezekano wa kuuzwa kwa hekalu lake. Lakini haitawezekana kuzuia."
Akiongea kwenye simu kutokea gerezani mjini Nevada, alimshutumu vikali binti huyo kwa kuteketeza fedha zake kwa ulevi na kuishi maisha ya anasa.
Chanzo kilisema: "O.J. amekuwa akigombana na Arnelle mara kwa mara kuhusu ulevi, na amejaribu bila mafanikio kwa miaka kadhaa kumuoza ili atoke kwenye jumba lake.
"Kitu pekee anachoweza kufanya ni kukaa na kunywa vodka hata wakati wa asubuhi."
"Arnelle ana pepo la kuzurura na kufanya manunuzi kwenye maduka. Hicho ndio kitu pekee kinachoweza kumtoa ndani. Manunuzi yote hayo ya vitu visivyo na umuhimu amekuwa akitumia fedha za baba yake.
"Pia amekuwa akiwaita nyumbani marafiki zake wote na kuwapeleka kwenye migahawa ya gharama na kuwanunulia vinywaji na vyakula."
Binti yake huyo anadaiwa ana mpango wa kununua nyumba mjini Los Angeles kwa kutumia fedha hizo za baba yake.
Vyanzo vimeeleza: "Matendo yake haya hakika ni kisasi dhidi ya baba yake ambaye miaka ya nyuma aliitelekeza familia na kujikita kwenye maisha ya ovyo na tabia chafu akishirikiana na marafiki wabaya na wanawake wasiokuwa na msimamo."
Akifahamika kama 'Juisi', OJ Simpson alikuwa mmoja wa wanamichezo waliotokea kupendwa akiwa na rekodi nzuri na anayeelekea kuwa bilionea.
Lakini vyote hivyo vilibadilika usiku wa Juni 12, 1994, baada ya kufanya mauaji ya watu wawili, mke wake wa zamani na rafiki yake, ambao walikutwa wamekufa kando ya njia ya waenda kwa miguu nje ya jumba lake jirani na Sunset Boulevard.
Simpson baada ya muda mfupi alikamatwa baada ya msako mfupi wa polisi kwenye mitaa ya Los Angeles, akiendesha gari kwa mkono mmoja huku mkono mwingine akiwa ameshikilia bastola aliyoielekezea kichwani kwake akitishia kujiua.
Jaji baadaye akamtia hatiani kwa mauaji ya watu wawili katika kesi iliyorushwa sana na vituo vya televisheni, ambapo aliamriwa kulipa fidia ya Pauni milioni 18.8 kwa madhara aliyosababisha.
Miaka 13 baada kufutiwa mashitaka ya mauaji, akatiwa hatiani kwa kosa la utekaji nyara na uporaji wa kutumia silaha pamoja na kumiliki silaha za maangamizi ndipo akahukumiwa kifungo cha miaka 33 jela anachoendelea kutumikia mpaka sasa.

No comments: