Wanaume watatu, Dokta, Mwanasheria na Mwendesha baiskeli wamekaa kwenye Pub moja maeneo ya Kinondoni Studio wakipata kilevi.
Baada ya muda kidogo huku kilevi kikianza kukolea, Dokta akasema, “Unajua kesho ni anivesari yetu. Nimemnunulia mke wangu pete ya almasi na gari aina ya Toyota Vitz. Nimefanya hivyo kama hatoipenda pete basi walau ataipenda Vitz, na atajua kuwa nampenda.”
Kisha Mwanasheria naye akasema, “Kwenye anivesari yetu mwaka jana nilimnunulia mke wangu mkufu wa dhahabu halafu nikampeleka London kwa matembezi. Nimefanya hivyo ili kama hakupenda mkufu basi walau atafurahia safari ya London, na atajua kuwa nampenda.”
Naye Mwendesha baiskeli akapiga funda moja la bia na kusema, “Kwenye Anivesari yangu nilimnunulia jimama langu vipodozi na bastola. Nimefanya hivyo ili kama hakupenda vipodozi basi ajipige risasi ili asiwatishe watu kwa sura yake mbaya.” Mh, makubwa…
No comments:
Post a Comment