BREAKING NEWS!!
Habari zilizotufikia zimesema kuwa Mahakama Kuu mkoani Arusha imetengua ubunge wa Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema baada ya kuridhika na tuhuma dhidi yake.Katika kesi hiyo, Lema alikatiwa rufaa na mpinzani wake, Dk. Batilda Buriani ambaye alidai kwamba katika kampeni za uchaguzi wa jimbo hilo, Lema aliongea maneno ya kumkashifu kinyume na sheria ya uchaguzi ambapo katika moja ya kashfa hizo anadaiwa alisema kuwa Dk. Batilda ni Mzanzibari.
Baada ya kutolewa hukumu vyanzo vya habari zimemnukuu Lema akisema kuwa hukumu hiyo ina mkono wa vyombo vya dola ambavyo vimeshinikiza ashindwe kesi hiyo.
Imeripotiwa kuwa hakukuwa na vurugu zozote nje ya mahakama hiyo mara baada ya hukumu kutolewa.
HABARI ZILIZOPATIKANA BAADAYE zinasema kuwa Lema amesema hatakata rufaa kwa sababu hataki kuitwa mbunge wa rufaa.
No comments:
Post a Comment