Kuna mambo mengi ya kufanana kati ya Steven Kanumba na Edward Sokoine. Ukiacha wanavyofanana kiasi, lakini wamekuwa na matukio mengi ya asili yanayoingiliana. KWANZA: Mwaka aliozaliwa Kanumba, 1984 ndio mwaka aliofariki Sokoine. PILI: Mwezi aliofariki Sokoine Aprili ndio mwezi aliofariki Kanumba wakitofautiana kwa siku tano tu. Sokoine alifariki Aprili 12 wakati Kanumba kafariki Aprili 7. TATU: Wakati Kanumba Januari 8, 2012 akisherehekea miaka 28 tangu kuzaliwa kwake, Taifa linaadhimisha miaka hiyo hiyo Aprili 12, 2012 tangu kifo cha Sokoine.
Muda wa kazi kwa mujibu wa Sheria ya Kazi ya mwaka 2004 ni masaa 9 kwa siku. Yakizidi sana ni masaa 12 kwa siku ambapo masaa matatu yanayoongezeka kutoka 9 huhesabiwa kama muda wa ziada (Overtime). Ni makosa kwa mwajiri kumshawishi ama kumlazimisha mfanyakazi kufanya kazi zaidi ya hapo kisheria. Siku za kufanya kazi kwa wiki ni tano tu (5), hivyo kufanya jumla ya masaa ya kufanya kazi kwa wiki kufikia 45. Kinyumbe cha hapo mfanyakazi unadhulumiwa haki yako na unatakiwa kushitaki upate haki.

No comments:
Post a Comment