Mv Liemba ndio meli kongwe zaidi duniani iliyoundwa nchini Ujerumani mwaka 1913. Tangu wakati huo meli hiyo imeendelea kufanya kazi mpaka sasa ikisafirisha abiria kwenye Ziwa Tanganyika. Mwaka 2013, meli hiyo itatimiza miaka 100 ambapo inasemekana kwamba waundaji wake, yaani nchi ya Ujerumani imepanga kufanya sherehe kubwa kwa pamoja na nchi ya Tanzania. Miaka kadhaa iliyopita, serikali ya Ujerumani iliomba kuichukua meli hiyo ambayo ni kielelezo cha mafanikio makubwa ya kiuhandisi nchini humo, ili iwekwe kwenye makumbusho ya nchi hiyo. Ombi hilo lilikataliwa.
No comments:
Post a Comment