Mwalimu mmoja mwenyeji wa mkoa wa Morogoro ndio kaanza kwenye shule moja ya msingi eneo la Mlandizi. Siku moja kawatoa wanafunzi wote wa darasa lake kwa ajili ya kipindi cha michezo. Wakati wote wakicheza soka kwa furaha, akamuona mtoto mmoja akiwa amesimama peke yake upande mmoja wa uwanja. Akamfuata na kumuuliza, “Vipi ungependa mimi niwe rafiki yako?” Yule mtoto akasita kidogo na kujibu, “Ndiyo”. Huku akiona dalili za kupata mafanikio ya kumfanya Yule mtoto awe na furaha, mwalimu akauliza tena, “Mbona umesimama peke yako?” Yule mtoto akajibu, “Unajua, mimi ndio goli”. Duh, mwalimu hoooooi…
No comments:
Post a Comment