CHEKA TARATIBU...

Wagonjwa watatu wa akili kwenye hospitali moja walipewa mtihani kujua kama wamepona au la. Atakayefaulu mtihani basi anaruhusiwa kuondoka hospitalini hapo na kurejea kwao. Atakayeshindwa, ataendelea kubai hapo kwa miaka mingine mitano. Dokta akawachukua wagonjwa hao watatu na kuwapeleka juu kwenye ubao wa kurukia kwenye bwawa la kuogelea ambalo halikuwa na maji wakati huo. Akamwamuru mgonjwa wa kwanza kuruka. Yule mgonjwa akaruka akitanguliza kichwa na alipotua akavunjika  mikono yote miwili. Mgonjwa wa pili akaruka na kuvunjika miguu yote miwili. Mgonjwa wa tatu akachungulia chini na kugoma kuruka. Dokta akasema kwa sauti, "Hongera! Umefanikiwa kupata ruhusa ya kutoka hospitali. Lakini kwanza nieleze kwanini umegoma kuruka?" Yule mgonjwa akajibu, "Dokta, mie sijui kuogelea!" Dah, kaazi kweli kweli...

No comments: