ALIYEUA MAMIA YA WATU AKIWAMO MJAMZITO ALILIA MSAMAHA...

KUSHOTO: Mansion alivyokuwa mwaka 1971 (juu) na alivyokuwa mwaka 1970. KATIKATI: Mansion akiwa gerezani mwaka 2011. KULIA: Sharon Tate (juu) na Mansion anavyoonekana kwenye picha za hivi karibuni.
Nywele zake zinaweza kuwa zimebadilika sana kwa kipindi chote alichokuwa akitumikia adhabu yake jela, lakini alama ya mchoro kwenye paji la uso wake bado iko vilevile.
Huyu si mwingine bali ni muuaji wa halaiki Charles Manson kama anavyoonekana kwenye picha alizopigwa hivi karibuni akiwa gerezani zilizotolewa hadharani na Mamlaka ya Magereza ya California wiki moja kabla ya kusikilizwa shauri lake la kumi na mbili la maombi ya msamaha kwa wafungwa (Parole).
Zinamuonesha Mansion mwenye miaka 77 akiwa amefuga nywele zake zenye rangi ya kijivu sasa. Picha yake ya mwishi ilitolewa hadharani miaka mitatu iliyopita akionekana amenyoa nywele kichwani.
Alama ya mchoro kwenye paji la uso wake katika picha hizi za sasa inaonekana kutofautiana na ile ya kwenye picha za miaka ya 1970.
Mansion amekuwa gerezani tangu alipotiwa hatiani kwa mauaji yaliyofanywa na wafuasi wake mwaka 1969 mjini Los Angeles.
Miongoni mwa waathirika wa mauaji hayo ni pamoja na Sharon Tate, mwigizaji aliyekuwa mjamzito wakati huo, mke wa Mwongozaji wa filamu Roman Polanski.
Mwendesha mashitaka alisema Mansion na wafuasi wake wanaojihusisha na dawa za kulevya, wanaojiita familia walijaribu kuanzisha mbio za kivita.
Bodi ya Parole ilitupilia mbali ombi lake la mwisho mwaka 2007, ikisema aliendelea 'kuonekana hatari kwa wengine na kwamba angeweza kumdhuru yeyote atakayekabiliana naye mbele yake'.
Katika miaka ya karibuni, Mansion alihukumiwa kwa kosa la kumtishia mlinzi na Oktoba mwaka jana, kwa kumiliki silaha yenye ncha kali mithili ya peni.
Familia ya Tate imechapisha kitabu kuhusu mauaji hayo ambacho wanasema wamekusudia kuishawishi magereza isimwachie huru Mansion.
Mwaka jana alivunja ukimya wa miaka 20 kwa mahojiano wakati wa maadhimisho ya miaka 40 tangu mauaji ya Tate. Alijitambulisha kama ‘mtu mbaya ambaye aliwafyatulia risasi watu’.
Katika moja ya mahojiano aliyofanya katika miaka ya 1980 aliwahi kusema: “Unatakiwa kujikubali mwenyewe kama Mungu. Unatakiwa kujigundua wewe ni shetani zaidi kuliko ulivyo Mungu, wewe ni kila kitu na wakati huohuo si kitu kabisa.”

No comments: