WALIOKUFA AJALI BASI NA TRENI MOROGORO WAFIKIA WATANO
Idadi ya watu waliokufa katika ajali iliyohusisha
basi na treni katika eneo la Kibaoni, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro
imeongezeka na kufikia watano baada ya dereva wa basi kufariki wakati akipatiwa
matibabu.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mussa Marambo amesema tukio hilo limetokea baada
ya basi lenye namba za usajili T837 CTM lililokuwa likienda Morogoro kukatiza
reli na kugonga treni.
Watu 25 wamejeruhiwa
katika ajali hiyo baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugonga treni
yenye nambari za usajili 88U3 ililokuwa linatokea mkoani Dodoma kuelekea
Morogoro.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Dennis Ngaromba ameelezea hali za wagonjwa
kuwa zinatofautiana ila bado wanaendelea na matibabu lakini pia ameeleza kuwa
wanakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo matatizo ya umeme hali iliyofanya
baadhi ya wagonjwa kuhamishwa hospitalini hapo.
Comments