HIVI NDIVYO BASI LILIVYOGONGA TRENI NA KUUA WATU WATANO TABORA


Watu watano wamekufa papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya DON’T WORRY kugonga Treni ya mizigo katika makutano reli na barabara kuu katika eneo la Malolo, nje kidogo ya mji wa Tabora.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana wakati basi hilo lilipokuwa likipita katika makutano ya Barabara Kuu ya Tabora-Kigoma na Reli ya Kati (Tabora na Kigoma).
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo dereva wa basi la DON’T WORRY alikuwa katika mwendo kasi kabla ya kugundua kuna treni inakuja na hivyo kuamua kukwepesha gari pembeni lakini likamshinda na kupinduka katikati ya barabara ndipo ajali hiyo ikatokea.
Baada ya ajali hiyo, dereva huyo akatoroka katika eneo la tukio huku majeruhi na marehemu wakipelekwa hospitalini.
Wawakilishi wa Shirika la Reli nchini (TRL) wamewakumbusha madereva kuwa waangalifu na alama za barabarani ili kuepusha ajali.

No comments: