AZAM TV YAZINDUA STUDIO ZA KISASA


Rais Jakaya Kikwete leo atakuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa studio ya kisasa ya Azam Tv itakayojulikana kama Uhai Production iliyopo eneo la Tabata kando ya barabara ya Mandela.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na uzinduzi huo, Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema studio hiyo itakuwa ni ya kisasa na haifanani na studio yoyote ya chombo chochote cha habari hapa Tanzania.
Aidha alisema hadi kukamilika kwa ujenzi wa studio hiyo zaidi ya dola za kimarekani milioni 31 zimetumika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uendeshaji, Yahya Mohamed amesema kuwa hadi kukamilika kwa ujenzi wote wa studio hiyo kutakuwa na studio tatu ambapo kwa sasa moja tu ndio iliyokamilika na zingine mbili bado zinaendelea na hatua za ujenzi.

No comments: