Mwanaume mmoja aliyejifanya msamaria mwema amembaka
mwanamke mwenye ulemavu wa kuona kwenye moja ya Stesheni zenye pilika nyingi
nchini Uingereza.
Wapelelezi wameweka hadharani picha za kamera za
CCTV za mtu ambaye wanataka kuongea naye kuhusiana na tukio hilo lililotokea
kwenye Stesheni ya Waterloo, mjini London.
Polisi wamesema mwathirika huyo aliingiliwa kimwili
ba mwanaume huyo ambaye alijitolea kumsaidia wakati akishuka kwenye treni
sambamba na mbwa wake anayemwongoza muda mfupi kabla ya Saa 4 asubuhi ya
Jumatano Desemba 3, 2014.
Mpelelezi Konstebo Suleman Yazdani alisema:
“Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kwenye treni ya Northern Line inayofanya
safasi zake kusini akiwa na mbwa wake anayemwongoza na sanduku lake dogo.
“Wakati akisogea kutaka kushuka kwenye treni hiyo
katika Stesheni ya Waterloo, ndipo akagundua kuna mtu yupo karibu yake.
“Mwanaume huyo akajitolea kumsaidia mlemavu huyo
kushuka kwenye treni hiyo, na kumshikilia.
“Hatahivyo, badala ya kumsaidia mwathirika wake,
mwanaume huyo akamwingilia kimwili mwanamke huyo kabla ya kutoweka eneo ya
tukio.”
Abiria mwingine alifika kumsaidia mwanamke huyo, na
kumsindikiza hadi kwenye sehemu ya kukatia tiketi ambako aliripoti tukio hilo
kwa wafanyakazi wa hapo.
Wapelelezi wamesema wanafuatilia simu kadhaa kutoka
kwa watu mbalimbali kuhusiana na tukio hilo, na, baada ya kupitia picha za
CCTV, wameweka hadharani picha ya mtu ambaye wanaamini atakuwa na taarifa
kuhusu kilichotokea.
Yazdani alisema: “Mtu huyo ambaye ametenda uhalifu
huo alijifanya kama msamaria mwema, kabisa ili kuweza kutumia fursa ya kufanya
shambulio la ubakaji kwa mwathirika wake huyo.
“Tunafanya kila linalowezekana kuhakikisha treni za
ardhini ni sehemu ambapo wanawake wanaweza kusafiri bila hofu ya tabia matukio
ya ubakaji yasiyotakiwa na tumedhamiria kumsaka mtu huyo aliyehusika na
shambulio hili.
“Huyu ni nani kwenye picha? Nafikiri anaweza kuwa
na taarifa ambazo zinaweza kutusaidia.”
No comments:
Post a Comment