MKE ASIMULIA JINSI ALIVYOBAKWA MARA 300 NA MUMEWE

Mwanamke mmoja amesimulia mkasa wake wa kutisha baada ya kugundua mumewe alikuwa akimbaka kwa siri wakati mwanamke huyo akiwa amelala huku akijirekodi wakati akifanya unyama huo.

Sarah Tetley, mkazi wa Melton Mowbray, Leicestershire, alipambana mshituko wa mashambulio hayo na msongo wa mawazo hadi kufanikisha mpenzi wake huyo wa zamani kwa sasa Charlie Tetley kuhukumiwa kifungo baada ya mashambulio hayo ya kuogofya ambayo yalifanyika kwenye chumba chao walichokuwa wakilala.
Mwanamke huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 26 aliweka hadharani habari yake kwa matumaini kwamba itawasaidia waathirika wengine wa vitendo kama hivyo vya udhalilishaji.
Sarah alidhani amebahatika kufunga ndoa yenye amani pale alipokutana na Charlie Tetley kwenye baa wakati huo akiwa na umri wa miaka 18.
Japo Charlie alikuwa mkubwa zaidi yake kwa miaka minane, wapenzi hao walifanya haraka na kuanzisha uhusiano huo wa kimapenzi.
Mnamo mwaka 2009,  walikamilisha familia yao pale Sarah alipopata ujauzito wa binti yao, ambaye sasa ana umri wa miaka minne.
Lakini taratibu, tabia ya Charlie ikaanza kuwa mbaya zaidi na alifikia hata kumwambia Sarah angekuwa wapi kama asingeolewa naye na jinsi ya kuishi na mtoto wao.
Licha ya baadhi ya mapungufu kuhusu tabia yake, Sarah alikubaliana na ombi ya rafiki yake huyo wa kiume la kuwa wapenzi, akiamini kwamba ndoa itarekebisha kasoro zote hizo katika mahusiano yao.
Hivyo basi wapenzi hao wakafunga ndoa mwaka 2011 kwenye kanisa moja mjini humo mbele ya wanafamilia wote na marafiki.
Badala ya kuimarisha kifungo chao, Charlie, ambaye sasa ana miaka 34 na kufanya kazi kwenye biashara ya baba yake, akawa mbali zaidi na Saraha baada ya ndoa.
Alikataa kabisa kumruhumu mkewe kutumia kompyuta yake na mara kwa mara alijifungia ndani ya chumba chao wakati wa jioni.
Sarah alihofia mumewe alikuwa na mahusiano na mwanamke mwingine kwa siri, lakini ukweli wa hilo ulikuwa mbaya zaidi ya hapo - alikuwa akimbaka wakati akiwa amelala usiku na kurekodi 'ushenzi' wake huo.
Sarah alikuja kugundua asubuhi moja pale alipoamka na kukuta Charlie akiendelea na zoezi lake la kumbaka.
Pamoja na kumbaka mkewe, Charlie aliweza kujirekodi akimdhalilisha Sarah kwa kutumia vitu mbalimbali vya ndani ya nyumba.
Alieleza: "Wakati nilipokuwa nikifikiri, nilijifanya kama nimelala fofofo na kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.
"Aliacha haraka sana na kutoweka chumbani na kushuka ngazi na kwenda kutazama upuuzi kwenye televisheni."
Baada ya mumewe kuondoka kwenda kazini, Sarah alikwenda nyumba ya jirani yake na kuwaelezea kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Jirani yake huyo akamshauri Sarah kuripoti tukio lake hilo kwa polisi na maofisa walifika mara moja kwa ajili ya kuchukua taarifa zaidi.
Sababu ya unyeti wa shambulio hilo, polisi hao walikamata laptop ya Charlie, kamera ya video na Xbox.
Wakati maofisa wakiendelea na msako wao, Sarah akagundua vifaa saba vya kuhifadhia taarifa vilivyokuwa vimefichwa chini ya kipande cha samani ndani ya chumba chao cha kulala na kisha kuvikabidhi kwa ajili ya uchunguzi.
Baada ya kukagua vihifadhio hivyo na kompyuta, polisi wa Leicestershire wakagundua picha za kutisha za ngono.
Aliondoka na maofisa hao kwenda kuandika rasmi maelezo kwenye kituo kimoja cha polisi na siku iliyofuatia wakamkamata Charlie na kumfungulia mashitaka ya makosa matatu ya ubakaji na mawili ya shambulio kwa kupenyeza vitu.
Alieleza: "Walinieleza wamegundua lundo la video zikimwonesha Charlie akinibaka na kunidhalilisha.
"Ofisa huyo alisema zilikuwa zinakera mno na kwamba nilikuwa nahitajika kwenda kituoni kwa uchunguzi na kuchukuliwa vipimo sababu ya uhalisia wa shambulio lenyewe na kwamba nilionekana nikiwa na hali mbaya kwenye video hizo."
Sarah alichukuliwa sampo za nywele, damu na mkojo, lakini vyote damu na mkojo wake havikuonesha uhusiano wowote na Charlie na sampo ya nywele zake haikuthibitisha chochote.
Kisha miezi michache baadaye, Sarah aliitwa tena katika kituo cha polisi na kutakiwa kutazama baadhi ya matukio 300 yaliyorekodiwa kwamba Charlie kwa miaka mingi alikuwa akimdhalilisha.
Maofisa wa polisi walimtaka atazame picha hizo za video kabla ya kuanza kwa kesi dhidi ya mumewe.
Alieleza kwamba amejawa na hofu kutokana na kile alichokiona kwenye picha hizo za video.
Ingawa video hizo, ambazo zilipigwa kuanzia Januari 2011 hadi Desemba 2012, hazikuwa nzuri kutazama, zilikidhi kile ambazo polisi walitaka kuthibitisha kwamba Charlie alikuwa na hatia ya kumbaka mke wake.
Mnamo Machi 28, 2014, Charlie alifikishwa katika Mahakama Kuu ya Leicester na kupatikana na hatia katika mashitaka matano ya ubakaji, kujaribu kubaka, mashitaka manane ya udhalilishaji kwa njia ya kupenyeza, matatu ya udhalilishaji kijinsia na kumi ya kutengeneza picha zisizofaa za watoto.
Alihukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.

No comments: