Mshambuliaji machachari wa timu ya
soka ya Simba, Emmanuel Okwi, jana jioni amenusurika kifo baada ya kupigwa
kiwiko nyuma ya kichwa kwenye mishipa ya fahamu na kuzimia kwa dakika kadhaa
uwanjani.
Mkasa huo ambao umethibitishwa na
daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, ulitokea wakati wa pambano la ligi kuu ya
Vodacom baina ya timu hiyo na Azam FC lililopigwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam na kuisha kwa sare ya bao 1-1. Bao la Simba lilifunwa na Okwi wakati
lile la Azam likiwekwa kimiani na Kipre Tchetche.
Kwa mujibu wa Gembe, Okwi alipatiwa
huduma ya kwanza uwanjani hapo kabla ya kupelekwa kwenye zahanati iliyoko pia
uwanjani hapo na kasha baadaye kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kwa
matibabu zaidi.
“Ilikuwa mbaya sana na angeweza hata
kupoteza maisha,” alisema Gembe na kuongeza;
“Tuliendelea kumpatia matibabu
kwenye zahati ndogo uwanjani hapo mpaka aliporejesha fahamu ndipo tukaanza
kuelekea Muhimbili kwa matibabu zaidi yaliyochukua takribani masaa mawili. Ila
kwa sasa yuko vizuri.”
Hatahivyo kwa mujibu wa taarifa za
daktari, Okwi atakuwa nje ya uwanja kwa siku kadhaa wakati akiwa chini ya
uchunguzi kuangalia maendeleo ya afya yake. Hiyo ni pamoja na kuwa nje katika
ratiba ya mazoezi ya timu hiyo.
Matokeo mengine ya mechi za Ligi Kuu
zilizopigwa wikiendi hii:
Kagera Sugar 1 – 2 Ndanda FC
Stand United 0 – 1 Coastal Union
JKT Ruvu 1 – 1 Mgambo JKT
Ruvu Shooting 2 – 1 Mtibwa Sugar
Mbeya City 2 – 2 Prisons
Polisi Moro 0 – 1 Yanga
No comments:
Post a Comment