Mshiriki
kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago ameibuka kidedea katika Shindano la Tanzania Movie
Talents (TMT) lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City,
jijini Dar es Salaam.
Katika
shindano hilo ambalo washiriki 10 walikuwa wakizitolea macho Shilingi milioni
50, Mwanaafa aliweza kuzoa kura nyingi zaidi na hivyo kujiwekea kibindoni
mamilioni hayo na kuwatimulia vumbi washiriki wengine.
Awali
kabla ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotions, Johnson
Lukaza alitoa ahadi kwamba kampuni hiyo itajitolea kumsomesha mtoto Mwanaafa
ili aweze kufanikiwa kufikia malengo yake.
Mwanaafa
ndiye mshiriki mdogo kuliko wote katika shindano hilo lililoandaliwa na Proin
Promotions ambapo miongoni mwa majaji watatu, wawili walikuwa waigizaji maarufu
nchini, Single Mtambalike ‘Ritchie Rich’ na Yvonne Cherie ‘Monalisa’. Jaji Mkuu
alikuwa Roy Sarungi.
Mara
baada ya kutangazwa mshindi, Mwanaafa aliangua kilio cha furaha kuonesha
kutoamini kwamba amefanikiwa kunyakua mamilioni hayo huku akihaha huku na kule
kumtafuta mama yake jukwaani.
Hata
baada ya kuitwa na kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 na Mwenyekiti wa
Proin Promotions, Mwanaafa aliendelea kububujikwa machozi ya furaha kuonesha
kabisa kutoamini kinachotokea usiku huo.
No comments:
Post a Comment