WATU WANANE MBARONI KWA MABAKI YA MIILI YA BINADAMU

Watu wanane wamekamatwa kuhusiana na tukio la kutisha na kusikitisha ya kupatikana na viungo mbalimbali vya binadamu eneo la Mbweni Mpigi Majohe, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema hayo muda mfupi uliopita wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam kuhusianana tukio hilo lililotokea jana.
Kamanda Kova amesema kuwa jopo la wataalamu saba limeundwa kuchunguza tukio hilo na amethibitisha kuwa viungo hivyo vilivyokamatwa vilikuwa ni vya maiti, ambavyo hutumika na madaktari kwa elimu ya matibabu na utafiti.
Pia amekanusha kwamba gary jeupe aina ya pick-up lililoambatana na taarifa hizo likiwa limebeba mifuko ya plastiki halihusiki na tukio hilo, bali baada ya kuliona na kusikia harufu kali ikitoka humo, walioliona likielekea dampo wakadhani ni mojawapo ya magari yaliyobeba viungo hivyo.
|Wananchi wakalifukuza gari na walipomkamata dereva wakamlazimisha arudi dampo, akawa hana jinsi ila kwenda kituo cha polisi Bunju kujisalimisha,| a;isema Kova.
Akaongeza, "Zogo kubwa likafumuka kituoni hapo kiasi cha kuwalazimu polisi kutumia nguvu za wastani na kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao."
"Huyu dereva alikuwa kabeba mabaki… ila siyo ya binadamu… Alikuwa kabeba mabaki ya kuku akitokea kiwanda cha kuku cha Interchick," alifafanua Afande Kova na kuzua kichezo cha mshangao kutoka kwa waandishi wa habari hao.

No comments: