Serikali imesema iko katika mchakato wa kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Kurekebisha sheria kwa sheria 29 kandamizi zikiwemo za ndoa na mirathi.
Aidha iko katika utaratibu wa kuweka mfumo wa kisheria utakaoratibu shughuli zote za huduma ya msaada wa kisheria nchini.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akifanya majumuisho ya ziara ya siku nne aliyoifanya katika taasisi zinazotoa huduma ya msaada wa kisheria za mkoa wa Dar es Salaam.
Kuhusu sheria kandamizi alisema tayari wizara yake imeyafanyia uchambuzi wa kina kuhusu mapendekezo ya uwepo wa sheria hizo kandamizi ambazo zinakinzana na juhudi za kulinda na kutetea haki za binadamu.
Alisema pia serikali iko kwenye utaratibu wa kuweka mfumo wa kisheria utakaoratibu shughuli zote za huduma ya msaada wa kisheria nchini ambao unawajumuisha wadau wote wa utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria.
Aidha aliwashauri watendaji wa idara na taasisi za serikali ambao hawajaanza kuwatambua watoa huduma za kisheria ili kuhakikisha kwamba wananchi wanapata haki zao kwa wakati.
Kadhalika, aliwasihi wananchi wanaokabiliwa na migogoro mbalimbali kuwatumia vyema wasaidizi wa kisheria katika utatuzi wa migogoro na kuepuka kupelekwa mahakamani kwa migogoro ambayo ingeweza kusuluhishwa nje ya mahakama.

No comments:
Post a Comment