KESI YA WATUHUMIWA MTOTO WA BOKSI YAAHIRISHWA TENA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro bado imeendelea kuahirisha kesi  inayowakabili watuhumiwa  watatu wanaokabiliwa na shitaka la kusababaisha kifo cha mtoto Nasra Rashidi (4) kwa madai ya kutokamilika upelelezi.
Watuhumiwa hao ambao ni baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi (47) mkazi wa Lukobe pamoja na wanandoa Mariam Said (38) na Mtonga Omari (30) wote wakiwa ni wakazi wa mtaa wa Azimio, kata ya Kiwanja cha ndege.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Mary Moyo, mwendesha mashitaka  wa polisi, Aminata Mazengo aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine ya kutajwa tena kutokana na upelelezi wake kutokamilika.
Hakimu  Moyo alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hiyo hadi  Agosti 6 mwaka huu itakapofikishwa mahakamani hapo kwa kutajwa tena na kwamba jalada la kesi hiyo bado liko kwa mwanasheria wa Serikali. Watuhumiwa wote walirudishwa rumande.

No comments: