Polisi Mkoa wa
Kinondoni, imewakamata vijana wawili wanaodaiwa kujifanya waganga wanaotoa tiba
kwa wanawake, ambayo masharti yake ni kushiriki nao ngono bila kinga na kuacha
nguo za ndani, ili zifanyiwe dawa zaidi.
Akizungumza na waandishi
wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke,
Englibert Kiondo, alidai vijana hao Juma Hemedi (32) na Abrahman Mulsin, wote
wakazi wa Tandika, baada ya kushiriki ngono na wagonjwa wao huwaambia waache nguo
za ndani.
Kamanda Kiondo alidai
baada ya kupata malalamiko, Jeshi la Polisi lianzisha msako na kuwapekua
waganga hao, ambapo walikutwa na nguo za ndani za kike 22, ambazo alisema
zitakuwa ushahidi wa kuingiliwa kimwili kwa wanawake hao. Vitu vingine wanavyodaiwa
kukutwa navyo ni pembe, tunguli, makopo ya dawa na vibuyu.
“Sheria iko wazi, inasema mganga anapofanya
ngono kama uganga anakuwa amebaka, na hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya
Adhabu 130 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,” alisema Kamanda
Kiondo.
Kwa
mujibu wa madai ya Kamanda Kiondo, vijana hao wamekuwa wakijifanya waganga wa
tiba asili, husambaza vipeperushi sehemu mbalimbali za jiji kutafuta wateja.
Mbali na tiba hiyo ya kupata watoto, inayotolewa kwa kushiriki ngono na mganga,
Kamanda Kiondo alidai watuhumiwa hao wamekuwa wakidai kutibu magonjwa mengine
kama kisukari, vidonda vya tumbo, nguvu za kiume, kukuza maumbile, kupata kazi,
kufaulu mtihani, mvuto wa biashara, kumilikishwa jini na kupewa pete ya bahati.
No comments:
Post a Comment