Polisi
mkoani Rukwa inamshikilia baba mzazi
huku ikimsaka mama wa mtoto
mwenye umri wa mwezi mmoja, Denis Umera aliyefariki dunia kutokana na
kilichodaiwa ni ugomvi wa wazazi hao uliotokana na wivu wa mapenzi.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda
alisema kifo hicho kilitokea saa 11
alfajiri, Juni 2, mwaka huu kijijini Mlanda katika Wilaya ya Sumbawanga baada
ya mama aliyekuwa amembeba mwanawe huyo, kusukumwa na mumewe na kumkandamiza
mtoto.
Kwa
mujibu wa Kamanda huyo, wanandoa hao walikuwa wakipigana. Mama wa mtoto, Imelda
Sindani (25) alikuwa akimtuhumu mumewe kuwa na mahusiano ya kimapenzi na
wanawake wengine.
Hata
hivyo kulingana na maelezo ya Kamanda, wanandoa hao walikuwa na kawaida ya
kugombana mara kwa mara hasa wanapotoka kilabuni kunywa pombe.
Kulingana
na maelezo yaliyotolewa Polisi, ni kwamba mwanamke huyo alikuwa akimtuhumu
mumewe kwamba tangu ajifungue, alikuwa si mwaminifu kwenye ndoa.
Usiku
wa tukio hilo inadaiwa katika kupigana, mwanamume alimsukuma mkewe aliyekuwa
amebeba mtoto. Alianguka na kumkandamiza hali iliyosababisha maumivu makali na
kisha mtoto kufa papo hapo.
Mwaruanda
alisema mwanamke huyo baada ya kugundua kuwa mtoto wake amefariki dunia,
alishusha maiti na kuitelekeza na kisha kukimbilia kusikojulikana. Polisi inaendelea
kumsaka.
Kwa
upande wake, baba wa mtoto aliangua kilio kilichosababisha majirani kufika na
kumkamata, kisha kumfikisha Kituo cha Polisi ambapo anashikiliwa mpaka sasa
akisubiri hatua zaidi za kisheria.
No comments:
Post a Comment