TABORA WAONGOZA KWA MAUAJI YA VIKONGWE



Mkoa wa Tabora unaongoza kwa mauaji ya wanawake na vikongwe kunakotokana na kukithiri kwa imani za kishirikina.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa polisi jamii nchini, Mussa Ally Mussa akiwa katika kijiji cha Idudumo kata ya Miguwa wilayani Nzega kuwa mkoa wa Tabora unaongoza kwa mauaji ya wanawake kwa sababu mbalimbali ikiwepo za ushirikina.
Mussa akizungumza na jeshi la jadi la sungusungu alisema kuwa mkoa huo wa Tabora unapaswa kubadilika na kuachana na mauaji ya wanawake na vikongwe na tayari jeshi hilo la jadi kwa kushirikiana na polisi wamedhibiti mauaji hayo.
Alisema sababu za kuuawa kwa wanawake ni sababu ambazo si za msingi kwa jamiii na badala yake husababisha yatima ikiwa na kukatisha maisha ya watu.
Mussa alisema sungusungu wanapaswa kushirikiana na jeshi la polisi kwa nyakati mbalimbali ili kuhakikisha wahalifu wanakosa nafasi katika kufanya uhalifu huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzan Kaganda alitoa filimbi 12 zitakazosaidia kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho.

No comments: