MWIGIZAJI ADAM KUAMBIANA AFARIKI DUNIAHabari zilizotufikia muda mfupi uliopita ambazo hazijathibitishwa zinasema kwamba, mwigizaji na mwongozaji filamu maarufu nchini, Adam Philip Kuambiana amefariki dunia mchana huu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Kuambiana ambaye amejizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa mashabiki wa filamu nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, alikutwa na mauti baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya Sinza, Dar es Salaam.
Chanzo kingine cha habari kilisema kwamba, Kuambiana amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla akiwa ‘location’, na kwamba mwili wa marehemu upo Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge.
Miongoni mwa filamu zilizomtangaza mno Kuambiana ni ile ya “Fake Pastors” akiigiza sambamba na Vincent Kigosi ‘Ray’.
Pia amewahi kuongoza filamu kadhaa ikiwamo ya “Bad Luck”.
Taarifa zaidi na uhakika utazipata hapahapa baada ya muda mfupi ujao. Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina

No comments: