Serikali ya Marekani umeikabidhi Tanzania
mtambo wa mfumo wa mawasiliano wa masafa
marefu, utakaowezesha kuona vyombo vilivyopo majini.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Pereira Silima katika tukio la kukabidhiwa mtambo huo,
lililofanyika Dar es Salaam.
Alisema mtambo huo uliokabidhiwa, utasaidia
kuona vyombo vyote vilivyopo majini na
utasaidia kufanya mapinduzi na
utaangalia usalama maeneo ya pwani.
Pia, alisema mtambo huo, utasaidia kufichua
dawa za kulevya, ambazo zinasafirishwa baharini na suala la kupambana na uvuvi
holela unaofanyika baharini.
“Tunapenda kuwafahamisha watanzania wategemee
kuwa vijana wao watakuwa salama na dawa za kulevya kwani mtambo huu utafichua
kila kitu,” alisema Silima.
Aidha, aliishukuru serikali ya Marekani kwa
msaada huo na aliwaahidi kuutumia vizuri na kuulinda ipasavyo.
Naibu Mkuu wa Polisi, Abdulrahman Kaniki
katika maoni yake alisema mtambo waliopewa upo kidijitali zaidi, hivyo jeshi
limepanga kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wake ili kuwezesha kutumia mtambo huo.
No comments:
Post a Comment