ASKOFU ALIYETIMULIWA KWA KUTEMBEA NA MWANAKWAYA AGOMA KUACHIA NYUMBA...

JUU: Sheila Graziano. CHINI: Dk Reid akiwa na mkewe Ruth. KULIA: Askofu Dk Michael Reid.
Askofu ambaye aligoma kuachia nyumba yake wakati alipofukuzwa kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanakwaya kwa miaka minane, ameamriwa na mahakama kuhama.
Dk Michael Reid, mwenye miaka 69, alitumikia miaka 30 kama mchungaji wa daraja la juu katika Kanisa la Trinity,  lililoko Pilgrims Hatch, huko Essex, kabla ya mahusiano hayo na Sheila Graziano kuanikwa hadharani mwaka 2008.
Skendo hilo limetikisa kanisa hilo na waumini wake na likapelekea kutimuliwa kwa askofu huyo, ambaye alikuwa amefunga ndoa na Ruth, kwa zaidi ya miaka 30 wakati huo.
Lakini, licha ya kusaini makubaliano akiahidi kuondoka nyumbani hapo, ilipofikia wakati wa kuhama, ofisa huyo wa zamani wa polisi alikataa kutoka.
Hata pale kanisa hilo lilipomlipa Pauni za Uingereza 465,000 kwa ajili ya kumnunulia nyumba mpya ya kuishi bila kulipia kwa maisha yake yote, Dk Reid alikataa kuondoka.
Lakini sasa, baada ya kupeleka kesi hiyo Mahakama Kuu, kanisa hilo limeshinda amri ya kumlazimisha Dk Reid kuachia nyumba hiyo, inayofahamika kama 'Nyumba ya Ushuhuda', na kukabidhi kwa matumizi ya mchungaji mpya wa kanisa hilo.
"Hakuna haki," alilalamika Dk Reid wakati akiondoka mahakamani hapo baada ya hukumu ya kesi hiyo.
Mwanasheria wa kanisa hilo, Paul Adams, aliieleza mahakama hiyo lilijaribu kumwondoa Dk Reid katika Nyumba ya Ushuhuda tangu mwaka 2009.
Alifukuzwa mwaka mmoja kabla baada ya habari za mahusiano hayo kutawala vichwa vya habari na alishindwa madai yake katika mahakama ya kazi kuhusiana na hilo.
"Miaka kama minne baadaye, hakuhama na sasa anaendesha huduma nyingine katika Nyumba ya Ushuhuda," alisema mwanasheria huyo. "Dk Reid alitimuliwa siku nyingi katika ajira yake na Trinity linajaribu kurejesha haraka ardhi inayozunguka nyumba hiyo, ambayo inatakiwa kutumiwa na Mchungaji huyo."
Adams alisema alisaini amri mwaka jana, akiahidi kuondoka na kuhamia katika nyumba mpya ambayo kanisa lilikuwa linataka kuinunua kwa ajili ya matumizi ya Dk Reid.
Lakini Dk Reid alisema hakuwa na dhamira ya kuhama, sababu Nyumba ya Ushuhuda ilikuwa 'yake', mahakama hiyo ilielezwa.
Ilipelekea kanisa hilo kufungua madai, amri ya mahakama kumlazimisha mtumishi huyo kutelekeleza alichokuwa ameahidi.
Dk Reid alifanywa kuwa askofu nchini Nigeria mwaka 1995 na akatawala katika vyombo vya habari kwa kuongoza maandamano dhidi ya uamuzi wa BBC kuonesha kipindi chenye utata cha muziki cha Jerry Springer - The Opera.
Alianzisha kanisa hilo kama Peniel Pentecostal Church na alikuwa Mchungaji mkuu kutoka mwaka 1978. Kwa sasa anaongoza kanisa la What God Can Do Ministries.

No comments: