UHAI WA MFALME ABDULLAH WA SAUDI ARABIA SASA WATEGEMEA MASHINE...

Mfalme Abdullah bin Abdulaziz al-Saud.
Mfalme wa Saudi Arabia kitabibu 'amefariki dunia' kwa takribani wiki nzima na yuko katika mashine za kumsaidia mapigo ya moyo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo.

King Abdullah bin Abdulaziz al-Saud amekuwa katika hali mbaya tangu Jumatano ya wiki iliyopita, kwa mujibu wa mwandishi mmoja wa Saudi Arabia anayefanya kazi mjini London, na amekuwa haonekani hadharani kwa muda wote huo.
Mwandishi huyo, anayeshughulikia habari za kila siku Asharq Alawsat, alieleza kwamba madaktari walilazimika kutumia mashine maalumu kumzindua mara kadhaa.
Mtawala huyo mwenye miaka 89 aliripotiwa tu kuwa hai kwa msaada wa mashine maalumu ya kumsaidia kupumua, lakini viungo vyake halisi vimeshaacha kufanya kazi.
Hii ni mara ya pili vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimeripoti 'kifo' cha mfalme huyo katika miezi ya hivi karibuni.
Royal Court, ambayo inawakilisha familia ya kifalme ya Saudi Arabia, haijasema chochote kuhusu taarifa hizo.
Novemba mwaka jana, Shirika la Habari la Saudi lilitangaza kwamba Mfalme huyo anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo kujaribu kukaza pingili zilizolegea.
Akikoroga taarifa hizi, Asharq Alawsat aliripoti mfalme huyo alikuwa 'amefariki dunia' karibu wiki nzima baada ya kuwekwa kwenye mashine hizo.
Shirika hilo la habari lilisema alikaribia mauti, lakini hili lilitupiliwa mbali na Royal Court.
Mfalme huyo anasemekana kuwa anasumbuliwa na matatizo yanayoendelea kwenye mgongo wake.
Mwaka 2010 alifanyiwa upasuaji mara mbili nchini Marekani baada ya kusumbuliwa na pingili zake za mgongo.
Mfalme Abdullah, ambaye aliingia madarakani mwaka 2005 baada ya kifo cha Mfalme Fahd, alimteua kaka yake Mwana Mfalme mrithi Salman Juni 2012 baada ya kifo cha Mwana Mfalme mrithi Nayef bin Abdulaziz.
Mwana Mfalme Salman, ambaye amepitwa miaka 13 na Abdullah, tayari anawajibika kama msaidizi wake anapokuwa safarini. Cheo chake rasmi ni Naibu Waziri Mkuu.

No comments: