NDEGE YA ABIRIA YANUSURIKA KUGONGA KITU KINACHOELEA ANGANI...

Ndege ya abiria ilifikia hadi ukaribu wa ndani ya futi 300 za kugongana na kitu ambacho hakikutambulika kilichokuwa kikielea angani, wachunguzi rasmi wameelezwa.

Licha ya uchunguzi, Bodi ya Airprox nchini Uingereza, ambayo inachunguza ripoti za kosakosa ya karibu - haikueleza kitu hicho cha rangi ya 'bluu na njano' ambacho kilipita chini ya ndege hiyo aina ya Airbus 320.
Tukio hilo lilitokea Desemba 2, mwaka jana juu ya Baillieston, maili 13 mashariki mwa Uwanja wa Ndege wa Glasgow, katika takribani futi 3,500 kutoka usawa wa bahari.
Rubani huyo aliyepatwa na mshituko aliripoti hatari hiyo ya mgongano kuwa ni 'kubwa'.
Ndege hiyo ya A320 ilikuwa ikishuka katika Glasgow kwenye mazingira salama sambamba na jua kwa nyuma, ndipo marubani wote wa ndege hiyo walipoona kitu umbali wa takribani yadi 100 kutoka hapo.
Ripoti ya bodi hiyo ilisema: "Kitu hicho kilipita moja kwa moja sambamba kabla ya rubani yeyote kati yao hajapata muda wa kuchukua hatua za kuepuka au 'kukitambua kwa uhakika', ingawa wote walikubali kwamba kilionekana cha rangi ya bluu na njano) au shaba) na kwamba 'kilikuwa kikubwa' chenye eneo dogo la mbele.
"Mwongozaji huyo alieleza hakuwa akizungumza na yeyote zaidi katika eneo hilo na hakuna kilichokuwa kimeonekana kwenye rada."
Rubani huyo hakika alishitushwa na kuripoti kwamba kulikuwa na hatari 'kubwa' ya mgongano kufuatia tukio hilo la Desemba 2, mwaka jana.
Aliwaeleza kwenye mnara wa mawasiliano: "Kuna kitu kinapita sambamba nasi karibu kabisa. Je, umepata chochote katika eneo letu."
Walijibu: "Hakuna. Hatujapata chochote kwenye rada."
Marubani wote walielezea kitu hicho kama 'bluu na njano (au shaba) rangi yake kikiwa na eneo dogo mbele lakini kilikuwa 'kikubwa kuliko puto'."
Shirika la ndege lililohusika halikutajwa na waandishi wa ripoti hiyo.
Mashirika kadhaa hurusha ndege za Airbus 320 kutoka uwanja wa ndege na zinaweza kupakia hadi watu 220 - ingawa idadi hiyo hutofautiana kutokana na idadi ya viti.
Waandishi wa ripoti hiyo walisema hawakuweza kufanyia kazi kitu hicho kilikuwa nini hasa.
Waliandika: "Mwongozaji alieleza kwamba hakuwa akiongea na mwingine yeyote katika eneo hilo na kwamba hakuna kilichoonekana katika rada. Hatua za usakaji zilichukuliwa bila majibu na rubani huyo wa A320 alieleza dhamira yake ya kuishitaki Airprox..'

No comments: